Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kadinali akutwa na hatia ya ngono

43812 Pic+kadinali Kadinali akutwa na hatia ya ngono

Tue, 26 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Australia. Kadinali George Pell wa Kanisa Katoliki nchini Australia amekutwa na hatia za unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto.

Tukio hili linamfanya Kadinali huyo kuwa kiongozi wa kwanza mwenye  hadhi ya juu kabisa wa Kanisa kukutwa na hatia hii.

Taarifa zinasema kwamba Kanidali Pell aliwafanyia unyanyasaji vijana wawili  1996, lakini amekana kuhusika.

Mashtaka yalifunguliwa tangu Desemba  lakini huenda hayakuwekwa wazi kutokana na sababu za kisheria.

Pell mwenye umri wa miaka 77 anatarajiwa kuhukumiwa  keshon  Jumatano, lakini mawakili wake wanasema kua watakata rufaa hatia hiyo.

Hata hivyo  kadinali Pell amekanusha kuhusika na matukio yote na  sasa yupo katika mapumziko marefu wakati wote wa kesi hii ikiendelea.

Pell alikua katika mwaka wake wa kwanza katika kanisa la  Melbourne mwaka 1996 alipowafanyia unyanyasaji watoto , baada ya kuwaambia kuwa walikunywa mvinyo wa kanisa, aliwalazimisha kumfanyia vitendo visivyofaa kama adhabu yao.

Kanisa limepata fursa ya kusikia ushahidi kutoka kwa mmoja wa waathiriwa wa unyayasaji huo, huku  mwingine tayari ameshatangulia mbele ya haki.



Chanzo: mwananchi.co.tz