Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kadinali Pell aliyetuhumiwa kwa unyanyasaji kingono hatazikwa kwa heshima

Kadinali Pell Aliyetuhumiwa Kwa Unyanyasaji Kingono Hatazikwa Kwa Heshima Kadinali Pell aliyetuhumiwa kwa unyanyasaji kingono hatazikwa kwa heshima

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Kadinali wa Australia George Pell - ambaye akutwa na hatia baadaye kuachiliwa kwa unyanyasaji wa watoto kingono - hatazikwa mazishi ya heshima ya kiserikali katika jimbo lake la nyumbani ili kuepusha sintofahamu kwa waathiriwa wa unyanyasaji, Mamlaka za Victoria zimesema.

Mweka hazina huyo wa zamani wa Vatikani alifariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 81.

Ndiye Mkatoliki mwenye cheo cha juu zaidi Australia, na kasisi mkuu zaidi kuwahi kufungwa kwa makosa ya unyanyasaji kingono watoto.

Mazishi ya serikali hutolewa mara kwa mara kwa watu mashuhuri wa umma nchini Australia. Lakini Kiongozi Mkuu wa Victoria - ambapo Kardinali Pell alizaliwa na alitumia karibu nusu ya majukumu yake huko - alisema hakuna mazishi kama hayo yangefanyika huko.

"Sikuweza kufikiria jambo lolote la kufadhaisha zaidi kwa waathiriwa," Daniel Andrews aliwaambia waandishi wa habari siku ya Alhamisi.

Bw Andrews pia alisema kuna uwezekano wa kuhudhuria mazishi ya kasisi huyo. Maafisa wa New South Wales, ambako Kardinali alihudumu kama Askofu Mkuu wa Sydney, pia wamesema hawatatoa heshima hiyo, kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari vya ndani.

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese pia amekataa kusema iwapo atahudhuria mazishi ya kadinali huyo. Kadinali Pell alikuwa Mkatoliki mwenye nguvu zaidi wa Australia, lakini alitukashifiwa na watu wengi huko Australia kutokana na tuhuma zake za unyanyasaji.

Chanzo: Bbc