Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kadinali Pell aliwahi kumkosoa Papa Francis kwa ujumbe wa siri

Kadinali Pell Aliwahi Kumkosoa Papa Francis Kwa Ujumbe Wa Siri Kadinali Pell aliwahi kumkosoa Papa Francis kwa ujumbe wa siri

Fri, 13 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Kadinali mwenye utata George Pell aliwahi kundika kimemo cha siri akikosoa uongozi wa Papa akisema ni "janga", anasema mwandishi wa habari aliyeichapisha taarifa hiyo.

Kadinali huyo wa Australia, aliyefariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 81, alikuwa mmoja wa wasaidizi wakuu wa Papa Francis hadi alipojiuzulu ili kukabiliana na mashtaka ya unyanyasaji wa watoto kingono.

Ujumbe huo ulichapishwa kwenye blogu ya Vatikani kwa kutumia jina 'feki' mwaka jana. Ilielezea kwa kina kile mwandishi aliona kuwa ni kushindwa kwa Papa wa sasa na orodha ya vipaumbele vya kuchagua Papa ama uongozi ujao.

Katika waraka huo, mwandishi aliandika kwamba "Kristo anahamishwa kutoka katikati" ya Kanisa chini ya Papa Francis, na kwamba heshima ya kisiasa ya Vatikani ilikuwa "imepungua" chini ya uongozi wake.

"Watoa maoni, ikiwa kwa sababu tofauti...wanakubali kwamba papa huyu ni janga katika mambo mengi; janga," Ujumbe unasomeka.

Inasema kwamba maamuzi na sera za Papa Francis mara nyingi zilikuwa "sahihi kisiasa", na kumshutumu kwa kukaa kimya juu ya masuala ya maadili - kama haki za binadamu huko Hong Kong na China bara na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

"Kazi za kwanza za Papa mpya zitakuwa kurejesha hali ya kawaida, kurejesha uwazi wa mafundisho katika imani na maadili, kurejesha heshima ipasavyo kwa sheria na kuhakikisha kuwa kigezo cha kwanza cha uteuzi wa maaskofu ni kukubalika kwa mapokeo ya kitume," inaeleza.

Mwandishi wa habari wa Italia Sandro Magister, ambaye awali alichapisha ujumbe huo, siku ya Alhamisi aliambia Reuters Kardinali Pell "alitaka niichapishe".

Padre Joseph Hamilton, katibu binafsi wa Kardinali Pell, alikataa kutoa maoni yake kwa vyombo kadhaa vya habari, akisema "amejishughulisha zaidi na msiba wake".

Msemaji wa Vatican pia amekataa kutoa maoni yake.

Papa Francis atatoa ujumbe wa mwisho katika misa ya mazishi ya Kardinali Pell siku ya Jumamosi, kama ilivyo desturi kwa makadinali.

Mapema wiki hii, gazeti la The Spectator lilichapisha kile lilichosema ni makala ambayo Pell aliandika muda mfupi kabla ya kifo chake.

Katika kipande hicho, Kadinali Pell alielezea mashauriano ya Papa na waumini wa Kanisa Katoliki kuhusu masuala kama vile mafundisho ya kanisa juu ya ngono na jukumu la wanawake kama "ndoto yenye sumu".

Chanzo: Bbc