Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaburi la askofu lachimbwa usiku

17591 Pic+kaburi TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbozi. Waumini wa Kanisa la Tanzania Evangelistic Assemblies of God (TEAG) wamelazimika kuchimba kaburi la kumzika askofu wa kanisa hilo, Zakaria Mwakasaka usiku baada ya kuchelewa kupewa kibali kutoka uongozi wa Halmashauri ya Mbozi mkoani Songwe.

Mmoja wa waumini hao, Ayub Sanga alisema kutokana na kuhitaji askofu wao azikwe eneo la kanisani kwao lililopo Mtaa wa Mbugani wilayani Mbozi kutokana na kuwa muasisi wa kanisa hilo, walilazimika kuomba kibali halmashauri lakini walichelewa kukubaliwa na kuruhusiwa juzi usiku.

Alisema baada ya kukubaliwa usiku huo, walianza kuchimba ili kupata nafasi ya kujenga pasipo kuathiri ratiba ya maziko yaliyofanyika jana.

Akizungumzia suala hilo kwa njia ya simu, Ofisa Mtendaji wa Mamlaka ya mji mdogo wa Vwawa, Osika Mgani alisema utaratibu wa kisheria upo pale pale isipokuwa kilichotokea katika kanisa hilo waliomba kibali maalumu ili waruhusiwe kumzika askofu wao eneo hilo na kwamba hawatazika tena mtu mwingine.

“Wameruhusiwa kwa kibali maalumu na kwa sharti la wao kuwaelimisha kwamba hawaruhusiwi kuzika ndani ya mji, huyu (askofu amezikwa) kutokana na sababu walizozitoa kwamba kwa ndiye muasisi wa kanisa lao, ndiyo maana wamekubaliwa,” alisema Mgani.

Mamlaka ya Mji wa Vwawa imepiga marufuku kuchimba makaburi ndani ya mji lakini katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja familia moja ilizika ndugu yao baada ya kupata kibari.

Chanzo: mwananchi.co.tz