Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KKKT Kusini wapata Askofu mpya

Kkkt Askf Kusin.png KKKT Kusini wapata Askofu mpya

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki limemtangaza Mchunguji Yeriko Ngwema kuwa Askofu Mkuu Mpya wa dayosisi hiyo ya Kusini, baada ya aliyekuwa Askofu katika dayosisi hiyo Lucas Mbedule kustaafu kwa hiari. - Askofu Mbedule alistaafu mapema Machi mwaka huu kutokana na kuwepo kwa migogoro ya kiutendaji katika dayosisi hiyo ya Kusini Mashariki, ambapo ilimlazimu kustaafu kwa hiari. - Mchunguji Ngwema alitangazwa kuwa Askofu mkuu Mteule katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa SINODI, ambao ulifanyika Julai 17 na 18, 2023 katika kanisa kuu la dayosisi hiyo Mtwara, ambao ulisimamiwa na Askofu Shoo. - Akizungumza katika Ibada ya kufunga mkutano huo, Askofu Shoo aliwataka viongozi wateule katika dayosisi hiyo kuachana na yale ambao waliamua nyuma na kusonga mbele kwa ajili ya kulijenga kanisa. - Akizungumza mara baada ya kuteuliwa kuwa Askofu Mkuu, Mchunguji Yeriko amemshukuru Mungu kwa namna ambavyo amemuita kumtumikia kupitia dayosisi hiyo ya Kusini Mashariki, huku akiwaomba washirika na viongozi wengine wa kanisa hilo kushikamana na kuwa chombo kimoja kumtumikia Mungu. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live