Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jumuiya na taasisi za kidini kuhakikiwa Tanzania

Wed, 15 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za kijamii na taasisi za kidini nchini iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani imesema itafanya uhakiki wa jumuiya na taasisi hizo nchi nzima kuanzia Mei 20 hadi 30 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa Jumatatu Mei 13,  2019 na Katibu Mkuu wa wizara jiyo Meja Jenerali Jacob Kingu imeeleza kuwa awamu ya kwanza ya zoezi la uhakiki itafanyika mikoa miwili  ya Dar es Salaam na Pwani.

Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa taasisi ambazo zitashindwa kufanya uhakiki kwa muda uliopangwa zitaondolewa kwenye orodha ya msajili.

“Taasisi ambazo zitashindwa kuhakikiwa kwa mujibu wa ratiba ya eneo husika zitalazimika kwenda makao makuu ya wizara jijini Dodoma kwa ajili ya uhakiki iwapo zitashindwa kufanya hivyo kwa muda uliopangwa zitaondolewa kwenye orodha.”

“Wakati wa usajili nyaraka zinazotakiwa kuwasilishwa ni cheti halisi na usajili kuvuli cha cheti hicho, Stakabadhi ya mwisho ya malipo ya ada iliyolipwa hivi karibuni, katiba ya jumuiya au taasisi husika iliyopitiwa na msajili, na barua inayothibitisha uwepo wa jumuiya au taasisi kutoka kwa afisa mtendaji wa mtaa ama kata mahali ilipo taasisi hiyo,” inaeleza taarifa hiyo.

 

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz