Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jopo la madaktari kumjadili Askofu Ruwa’ichi leo

75577 Pic+ruaichi

Fri, 13 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati hali ya afya Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam,  Mhashamu Yuda Thaddaeus  Ruwa’ichi ikiendelea kuimarika,  jopo la madaktari  leo Ijumaa Septemba 13, 2019 litakutana kuangalia uwezekano wa kumuondoa wodi ya uangalizi maalum (ICU).

Septemba 8, 2019 Askofu  Ruwa’ichi alifanyiwa upasuaji wa kuondoa damu kwenye ubongo katika Taasisi ya Mifupa (Moi) na hadi leo mchana alikuwa katika chumba hicho.

Akizungumza na Mwananchi ofisa uhusiano wa Moi,  Patrick Mvungi amesema jopo la madaktari saba wanaomuhudumia watakutana kuangalia hatua gani itafuta.

Mvungi amesema afya yake  inazidi kuimarika na tayari ameanza mazoezi ya kukaa na kusimama.

“Kila siku asubuhi inafanyika ibada kitandani kwake na leo kwa mara ya kwanza ameshiriki akiwa amekaa, hii inaleta matumaini makubwa na anaonekana anapata nafuu kwa uharaka.”

“Kitaalam madaktari wake wanaendelea kumuangalia na watakutana kuangalia hatua gani ifuatwe apelekwe HDU au moja kwa moja aende wodi ya kawaida,” amesema Mvungi

Pia Soma

Advertisement
SOMA ZAIDI

 > Magufuli amjulia hali Askofu Ruwa’ichi

> Askofu Ruwaichi afanyiwa upasuaji MOI

> VIDEO: Afya ya Ruwa’ichi yaimarika, aanza kula

Chanzo: mwananchi.co.tz