Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jimbo Kuu Katoliki Dar lapata maaskofu wasaidizi

Ef43b3fbca7830f91398fc9d553f42e6 Jimbo Kuu Katoliki Dar lapata maaskofu wasaidizi

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BABA Mtakatifu Fansisko amewateua mapadre wawili wawe maaskofu wasaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kuanzia jana.

Walioteuliwa ni Padre Henry Mchamungu na Padre Stephano Musomba wa Shirika la Waagustiniani (O.S.A).

Kwa mujibu wa taarifa kwa ummna iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima Mhashamu Askofu Mteule, Henry Mchamungu alizaliwa Januari 18, 1965 Kijiji cha Legho Kilema jimboni Moshi.

Baada ya masomo ya upadre alipewa daraja takatifu la upadre Juni 24, 1994 na kuhudumu katika nafsi za utume Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.

Hadi uteuzi wake, Askofu mteule Mchamungu alikuwa mlezi wa Seminari ya Segerea, Dar es Salaam

Taarifa hiyo ya Kitima pia ilimwelezea Mhashamu Askofu Mteule Stephano Lameck Musomba kuwa alizaliwa katika Kijiji cha Malonji jimboni Mbeya Septemba 25, 1969.

Baada ya masomo ya upadre alipewa daraja takatifu la upadre Julai 24, 2003 kisha kuhudumu nafasi za utume shirikani na Jimbo Kuu la Dar es Slaam na Morogoro.

Hadi anateuliwa, Askofu Mteule huyo alikuwa Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili ya Mavurunza, Dar es Salaam pia akihudumu kama Katibu wa Shirika lake la Waagustiniani Kanda ya Tanzania.

Chanzo: www.habarileo.co.tz