Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Polisi lamuachia Mch. Masisi

Ceasar Masisi Jeshi la Polisi lamuachia Mch. Masisi

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mch. Ceasar Masisi wa Huduma ya Spirit Word Ministry Tanzania (SWMT), ambaye alikuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi cha Central, Dar es Salaam kwa siku 5 ameachiwa leo muda mchache uliopita kwa dhamana ya Polisi.

Kwa sasa anangaliwa afya yake na madaktari kwa kuwa afya yake ilianza kudhoofu akiwa ndani.

Mke wake ametuma ujumbe kwetu Askofu kupitia kwa Askofu mmoja akimshukuru kila mmoja wetu aliyeshiriki kumpazia sauti mume wake hadi akatolewa. Tunapenda pia kumshukuru Askofu ambaye hatutamtaja kwa jina aliyetushirikisha taarifa hizo na kutuomba kupaza sauti.

Kipekee tunapenda kumshukuru Msajili wa Taaasisi za Kiraia kwa usikivu na hekima iliyotumika. Tunamshukuru pia IGP, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam pamoja na wote walioshughulikia jambo hilo upande wa serikali.

Tunamshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ushirikiano uliotolewa na Wizara yake kuhusu suala hilo. Sisi viongozi wa Kanisa tunaunga mkono vita dhidi ya vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Hata hivyo, ilikuwa ni wajibu wetu kama viongozi wa Kanisa kutetea haki ya msingi ya Mch. Masisi ambayo ni haki ya kuishi na haki ya kujitetea mbele ya mahakama kwa mujibu wa sheria na ndio maana tunapinga vitendo vya kuwashikilia watuhumiwa kinyume cha sheria na kinyume cha Katiba.

Tunafanya utaratibu kama viongozi wa Makanisa ili kukaa na mhusika ili kumsaidia na kumshauri pale inapowezekana na mashauri hayo yatafanywa na viongozi walio na heshima katika jamii ya Kikristo ambao kwa pamoja tutawateua.

Kwa sasa tunaishauri familia ya Mch. Masisi kuwa watulivu wakati suala lake linashughulikiwa na viongozi wa Makanisa nchini kwa kushirikiana na serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live