Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jerry Muro achangisha Sh491 milioni ujenzi kanisa la KKKT

33870 Pic+muro Tanzania Web Photo

Fri, 28 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arumeru. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ameendesha harambee kukusanya Sh51 milioni ahadi Sh440 milioni za ujenzi wa jengo kubwa la kisasa la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Lyamungo mkoani Arusha.

DC Muro aliendesha harambee hiyo juzi kwa kunadi vitu mbalimbali ikiwamo mikungu ya ndizi, ng’ombe na kuku.

Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba watu mbalimbali kujitokeza kuunga mkono jitihada walizozianzisha za ujenzi wa kanisa hilo.

 “Huu ni wakati wa kuchangia maendeleo ya jamii ikiwamo maisha yetu ya kiroho na kiimani,” alisema Muro.

Alisema harambee hiyo aliyoianzisha itahitimishwa siku ya Pasaka Aprili  21 mwaka 2019.



Chanzo: mwananchi.co.tz