Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamii yakumbushwa kufundisha watoto maadili bila kuwabagua

IMG 4481.jpeg Jamii yakumbushwa kufundisha watoto maadili bila kuwabagua

Thu, 29 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Jamii mkoani Kilimanjaro imetakiwa kuchukua jukumu la kuwafundisha maadili watoto ili kukuza kizazi chenye nidhamu kwa manufaa ya Taifa.

Wito huo umetolewa na Sheikh wa Mkoa wa Kilimanjaro, Shaabani Mlewa wakati wa swala ya Eid el Adh’haa iliyofanyika Msikiti wa Sanya Juu wilayani Siha mkoani hapa leo Alhamis Juni 29, 2023.

Hiyo imetokana na baadhi ya watoto kuonekana wakifanya matendo mabaya mbele ya jamii ikiwemo unywaji pombe na kuvuta bangi huku jamii ikiwaangalia bila kuchukua hatua.

"Ni kweli zamani mtoto alipofanya kosa anaadhibiwa na mtu yeyote ili aache kosa hilo, lakini zama hizi mtoto akifanya kosa ukisema umuadhibu inakuwa umefanya kosa. Hivyo wazazi tubadilike, tuwalee watoto wetu kama zamani ili Taifa liwe na watoto wenye nidhamu," amesema Sheikh Mlewa.

Amesema pale anapoharibika mtoto wa jirani, maana yake pia umeharibikiwa na wewe. Pia amewataka Watanzania kuwa wamoja katika kudumisha amani ya nchi, na kama kuna jambo lizungumzwe kwa amani kwa faida ya Taifa.

Pia lmamu wa msikiti huo, Ally Mohammedi amewataka waumini kuendelea kufanya mambo mazuri yanayompendeza Mwenyezi Mungu.

Amesema kila mtu anafahamu nafsi yake, hivyo aisimamie nafsi hiyo iendelee kufanya mazuri yale yote aliyokataza Mungu ayatimize ili abaki salama duniani na akhera.

Chanzo: Mwananchi