Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo wakimbizi walivyofunga Ramadhani

Hivi Ndivyo Wakimbizi Walivyofunga Ramadhani Hivi ndivyo wakimbizi walivyofunga Ramadhani

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mwezi mtukufu wa Ramadhani unafikia ukingoni mwishoni mwa juma hili, huku mamilioni ya waumini wa kiislam duniani kote wakitarajia kuadhimisha sikukuu za Eid.

Hali wakati wa mfungo imekua tofauti kutokana na eneo fulani.

Lakini umewahi jiuliza wakimbizi katika kambi mbalimbali huwa katika wakati gani kipindi cha mfungo?

Mwandishi wa BBC David Nkya amefika Kigoma Magharibi mwa Tanzania na kuwakuta baadhi wakiwa katika maandalizi ya sikukuu ya Eid.

Wakimbizi hawa ambao wengi wanatokea DRC wanasema mwezi mtukufu wa Ramadhani hauwezi kufanana wakiwa katika sehemu hizi mbili, yaani kambini na nyumbani.

"Nikiwa nyumbani kipindi cha nyuma nilikua na uwezo wa kuamua futari iwe nini, sikukuu niende wapi, wanangu wavae nini, lakini nikiwa hapa kambini siwezi, tunakula kile tunachopewa, hatupo kwetu, tupo kwa watu, tumefadhiliwa, hatutegemei kila kitu kitakua sawa" anasema mmoja wa wakimbizi mwanamke ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Mkimbizi mwingine mwanaume yeye anasema "Kwa kawaida tulikua tuna utaratibu wa kualikana futari kama marafiki, lakini kwa sasa haiwezekani, natamani sana kuurudia utaratubu huu".

Kwa mujibu wa shirika la wakimbizi duniani UNHCR, kumekua na ongezeko la zaidi ya wakimbizi 7,600 kutokea DRC wanaoingia mkoani Kigoma tokea mwezi Machi mpaka sasa. Moja ya sababu kubwa ikitajwa kuwa ni ukosefu wa usalama Mashariki mwa Congo.

Hata hivyo afisa mmoja wa shirika hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema utaratubu wa kuwaandalia futari wakimbizi waislam hufanyika, licha ya kwamba sio wengi.

"Tuna utaratibu wetu wa kuandaa futari na daku, wakimbizi waislamu sio wengi sana, na hata sikukuu ya Eid tutafanya sherehe ndogo kwa ajili yao" anasema.

Kwa baadhi ya wakimbizi wenye uwezo, wameonekana wakinunua mahitaji mbalimbali ikiwemo nguo. Lakini wengi haswa wale ambao ndio kwanza wamefika wanaona hazitakua sherehe za kawaida na pengine kusisimua kama walipokua uraiani katika nchi zao.

Kushika saumu katika mwezi huu kunachukuliwa kuwa moja ya nguzo tano za Uislam ambapo sherehe za Ramadhan hudumu kwa takriban siku 29 ama 30.

Mwezi huu mtukufu kimsingi ni mfano wa nidhamu binafsi ambapo waumin hutumia muda huo kufanya sala, matendo mema, hisani na huduma za jamii ambayo kwa njia fulani huwaweka karibu na Mwenyenzi Mungu.

Chanzo: Bbc