Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hija yaanza katikati ya mgogoro wa Ghuba

70357 Pic+mahujaji

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zaidi ya Waislamu milioni 2.5 wataanza hija Ijumaa katika mji mtakatifu wa Kiislamu wa Mecca, Saudi Arabia, huku kukiwa na mgogoro katika Ghuba.

Makundi ya waumini yameshaanza kukusanyika Mecca ikiwa ni siku chache kabla ya hija, moja ya matukio muhimu katika kalenda ya Waislamu.

"Ni mara ya kwanza nimehisi kitu kwa hisia kubwa," alisema hujaji mwenye umri wa miaka 40 kutoka Indonesia, Sobar.

Zaidi ya mahujaji milioni 1.8 waliwasili jana Jumanne mchana, kwa mujibu wa mamlaka.

Makundi ya waumini kutoka sehemu mbalimbali duniani waliwasili wakiwa wamevalia kanzu nyeupe katika jiji hilo lililo magharibi mwa falme hiyo ya kihafidhina.

Mahujaji hao watapitia taratibu za kidini ambazo hazijabadilika tangu kuanzishwa kwa Uislamu karne 14 zilizopita.

Pia Soma

"Uislamu unatuunganisha. Wote tuko pamoja... ndio maana nimefurahi sana," alisema Leku Abibu, Mganda mwenye umri wa miaka 46 na ambaye ni mekanika aliyekuwa amevalia vazi la salwar kameez.

"Nafurahia hili hapa."

Hija ya mwaka huu inafanyika huku hali ikiwa haijatulia katika eneo la Ghuba, jambo linalozidishwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya  kwa meli za mafuta, kwa ndege isizo na rubani na kuingiliwa kwa safari za meli baharini.

Saudi, nchi yenye nguvu katika eneo la Ghuba, na mshirika wake Marekaqni wanaituhumu Iran -- mpinzani mkubwa wa Riyadh -- kuwa ndiyo inayohusika na mashambulizi hayo na hujuma dhidi meli za kibiashara.

Lakini Iran imekanusha madai hayo.

Licha ya kuharibika kwa uhusiano huo wa kidiplomasia baina ya Saudi na Iran, mahujaji wapatao 88,550 kutoka Iran wanatarajiwa kushiriki katika hija ya mwaka huu, kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim.

Chanzo: mwananchi.co.tz