Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye historia imeandikwa, Askofu Rugambwa apewa hadhi ya Ukardinali

Rugambwa 04828 Hatimaye historia imeandikwa, Askofu Rugambwa apewa hadhi ya Ukardinali

Sat, 30 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye historia imeandikwa. Baba Mtakatifu Francis amempa Hadhi ya Ukardinali Askofu Mkuu Protase Rugambwa katika viwanja vya Mt.Petro nchini Vatican leo Septemba 30, 2023.

Leo Maaskofu wakuu 21, wamepewa hadhi ya Ukardinali kutoka nchi mbalimbali duniani. Mmoja wao ni Protace Rugambwa, Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu katoliki Tabora. Kardinali Rugambwa anakua Mtanzania wa 3 kupata wadhifa huu mkubwa baada ya Baba Askofu Laurean Rugambwa, Mwadhama Polycarp Pengo na sasa Kardinali Protase Rugambwa.

Kardinali Protase Rugambwa ni mzaliwa wa Karagwe, Ukoo wa Abakaraza (Abarigi). Majina yake ya kifamilia ni Protase Abakaraza. Hilo la Rugambwa alipewa kama heshima kwa Askofu Laurean Rugambwa ambaye alifanya ziara Bukoba siku aliyozaliwa Protase.

Baba yake akasema kwa kuwa umezaliwa leo, siku ambayo Kardinali Rugambwa amekuja kwetu, basi utaitwa kwa jina lake. Basi akabatizwa na kuitwa Protase Rugambwa. Na kwa hakika jina hubeba tabia za mtu. Hatimaye nae amekua Kardinali kama mwenye jina lake.

Katika kuonesha mtamgamano wa Kanisa (Church compatibility) Askofu Rugambwa amesindikizwa Vatican na viongozi mbalimbali wa kanisa Katoliki na makanisa mengine. Mmoja wapo ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, Dr.Benson Bagonza (PhD) ambaye amekwenda Vatican kushuhudia tendo hili kubwa kwa mwana Karagwe mwenzie.

Askofu Bagonza alipopewa nafasi ya kusema neno kuhusu Kardinali Rugambwa amesema "Ni mtu ambaye hekima imemzidi kimo na utu umemtangulia mbele. Ni Mnyenyekevu lakini si Mdhaifu. Mwenye nidhamu lakini si muoga. Makardinali ndio Washauri wakuu wa Papa.

"Tumuombee Kardinali Rugambwa katika wajibu wake huu mpya wa kuwa Mshauri wa Papa"Hatimaye historia imeandikwa. Baba Mtakatifu Francis amempa Hadhi ya Ukardinali Askofu Mkuu Protase Rugambwa katika viwanja vya Mt. Petro nchini Vatican leo Septemba 30, 2023.

Leo Maaskofu wakuu 21, wamepewa hadhi ya Ukardinali kutoka nchi mbalimbali duniani. Mmoja wao ni Protace Rugambwa, Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu katoliki Tabora. Kardinali Rugambwa anakua Mtanzania wa 3 kupata wadhifa huu mkubwa baada ya Baba Askofu Laurean Rugambwa, Mwadhama Polycarp Pengo na sasa Kardinali Protase Rugambwa.

Kardinali Protase Rugambwa ni mzaliwa wa Karagwe, Ukoo wa Abakaraza (Abarigi). Majina yake ya kifamilia ni Protase Abakaraza. Hilo la Rugambwa alipewa kama heshima kwa Askofu Laurean Rugambwa ambaye alifanya ziara Bukoba siku aliyozaliwa Protase.

Baba yake akasema kwa kuwa umezaliwa leo, siku ambayo Kardinali Rugambwa amekuja kwetu, basi utaitwa kwa jina lake. Basi akabatizwa na kuitwa Protase Rugambwa. Na kwa hakika jina hubeba tabia za mtu. Hatimaye nae amekua Kardinali kama mwenye jina lake.

Katika kuonesha mtamgamano wa Kanisa (Church compatibility) Askofu Rugambwa amesindikizwa Vatican na viongozi mbalimbali wa kanisa Katoliki na makanisa mengine. Mmoja wapo ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, Dr.Benson Bagonza (PhD) ambaye amekwenda Vatican kushuhudia tendo hili kubwa kwa mwana Karagwe mwenzie.

Askofu Bagonza alipopewa nafasi ya kusema neno kuhusu Kardinali Rugambwa amesema "Ni mtu ambaye hekima imemzidi kimo na utu umemtangulia mbele. Ni Mnyenyekevu lakini si Mdhaifu. Mwenye nidhamu lakini si muoga. Makardinali ndio Washauri wakuu wa Papa. Tumuombee Kardinali Rugambwa katika wajibu wake huu mpya wa kuwa Mshauri wa Papa" Roma Locuta, Causa Finita. Roma ikishasema, mjadala umefungwa.!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live