Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

HIVI PUNDE: Askofu Desmond Tutu afariki dunia

Desmondtutu HIVI PUNDE: Askofu Desmnd Tutu afariki dunia

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askofu Mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu, mmoja wa viongozi wa vuguvugu la kupinga ubaguzi wa rangi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, Ofisi ya Rais imesema.

Alikuwa mkosoaji mkubwa wa mfumo wa kikatili wa makaburu wa nchi hiyo wa ukandamizaji dhidi ya Weusi walio wengi nchini humo.

Alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 1984 kwa kampeni yake ya upinzani usio na vurugu dhidi ya utawala wa wazungu wachache wa Afrika Kusini.

"Kufariki kwa Askofu Mkuu Emeritus Desmond Tutu ni sura nyingine ya msiba katika kuaga taifa letu kizazi cha Waafrika Kusini mashuhuri ambao wametuachia urithi wa Afrika Kusini uliokombolewa," Rais Cyril Ramaphosa alisema.

Taarifa kwa niaba ya familia ya Tutu ilimtaja kama mtu ambaye "aligeuza masaibu yake kuwa fursa ya kufundisha ili kuongeza ufahamu na kupunguza mateso ya wengine."

Ilisema: "Alitaka ulimwengu kujua kwamba alikuwa na saratani ya kibofu, na kwamba inapogunduliwa haraka ndivyo uwezekano wa kuidhibiti."

Taarifa hiyo iliongeza: "Hatimaye, akiwa na umri wa miaka 90, alifariki kwa amani katika Kituo cha Utunzaji cha Oasis huko Cape Town asubuhi ya leo.'

"Jasiri, mwenye neema, na anayejali ustawi wa wengine hadi mwisho.

"Kama Bi Tutu asemavyo, ingawa hakuwa na nguvu za kimwili, alikuwa na nguvu za ndani kama za simba."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live