Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gwajima asema kuna jambo video iliyosambaa mtandaoni

56400 Gwajima+pic

Thu, 9 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu Josephat Gwajima amesema kuna jambo nyuma ya video iliyosambaa mtandaoni inayomhusisha na vitendo visivyofaa na kuitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kutegua kitendawili cha aliyeitengeneza na kuisambaza.

Askofu huyo wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, alieleza hayo jana katika mkutano na waandishi wa habari ambao aliambatana na mkewe, ili kukanusha kuhusika na vitendo hivyo.

Video hiyo inamuonyesha mtu anayeonekana kuwa na sura kama ya kiongozi huyo wa kidini akiwa na mwanamke wakishiriki tendo la ndoa na ilisambaa kwa kasi jana, hasa katika mtandao wa Whatasap.

“Video hiyo imetengenezwa kwa lengo la kunichafua na kunivunjia heshima hasa kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020,” alisema Askofu Gwajima, ambaye amekuwa akikumbana na misukosuko dhidi ya mamlaka na mapambano dhidi ya wanasiasa.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika jana kanisani kwake, Ubungo na kuhudhuriwa na baadhi ya waumini, Gwajima alimuonya aliyeitengeneza video hiyo na kumtaka kurekebisha hali hiyo, la sivyo ataanza kumshughulikia kanisani kwake kuanzia Jumapili ijayo, huku akisisitiza kuwa safari hii itakuwa kali zaidi.

“Labda mjiulize ni mwanaume gani mwenye akili timamu anaweza kujirekodi akiwa faragha, halafu asambaze mwenyewe (video). Ile video imetengenezwa na wanajua wametumia teknolojia gani kutengeneza,” alisema.

Habari zinazohusiana na hii

“Najua mwakani ni uchaguzi na kuna watu wanajaribu kuzima sauti yangu. Sasa nawaambia, sizimiki na asitegemee kwamba amenidhalilisha, ndio kwanza ameonyesha kwamba mimi ni mwanaume wa kweli inapotokea tendo la ndoa naweza kufanya.”

Gwajima alisema anamjua aliyeitengeneza na kuisambaza.

Msemaji wa TCRA, Semu Mwakyanjala alisema polisi kitengo cha uhalifu wa mtandao ndiyo wenye jukumu la kuchunguza na kufuatilia suala hilo la kijinai.

Kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alisema jana kuwa uchunguzi umeanza na kuwataka wananchi kuwa watulivu.

Askofu Gwajima aliwahi kukumbana na tuhuma kama hizo mwaka juzi wakati msichana mmoja aliporekodiwa na kituo kimoja cha televisheni akidai kuwa alizaa na kiongozi huyo na baadaye kutekelezwa. Baadaye alikanusha.



Chanzo: mwananchi.co.tz