Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eneo la Ubatizo la Yesu kuwa kivutio zaidi 2030

UBATIZO WA YESU 5 Eneo la Ubatizo la Yesu kuwa kivutio zaidi 2030

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo Mto Jordan unakosa sehemu ya maeneo yake Kibiblia , lakini wageni wapatao 200,000 bado hutembelea kwenye kituo ambacho cha kitamaduni kwa ajili ya Ubatizo wa Kikristo katika Mto Jordan kila mwaka.

Nilitazama kikundi kutoka Marekani na Ulaya kikiingia katika maji ya matope na kupiga picha zao kwenye kingo za mto.



"Unapokuwa hapa lazima utembelee eneo hili. Ni sehemu ya historia," anasema Oliver mwenye shauku, kutoka Ufaransa. Mark kutoka Maryland anasema alikuja kwa ajili ya "imani, ili kuweza kutembea katika hatua za Yesu".

Mwezi huu ni mwezi wenye idadi kubwa zaidi ya mahujaji kwani waumini wa makanisa ya Kiorthodox wa Magharibi na Mashariki wanasherehekea Epiphany.

Kumbukumbu ya jinsi Wanaume watatu wenye hekima, au Mamajusi, walivyomtembelea mtoto mchanga aliyezaliwa Yesu, na kubatizwa kwake baadaye na nabii John.

Hivi karibuni, Jordan iloitangaza mpango kabambe wa dola milioni (£83m) wenye lengo la kuwaleta mamilioni ya Wakristo kutembelea eneo hilo al-Maghtas katika mwaka 2030, kusherehekea kile kinachoonekana kama mwaka wa 2,000 wa ubatizo wa Yesu Kristo.

Iliahidi kujenga kijiji cha Kibiblia na eneo kubwa zaidi la hija kwa Wakristo na kituo cha imani mbali mbali katika kanda hiyo, ikitambua kwamba Mto Jordan na mabonde yake pia vina umuhimu kwa dini za Wayahudi na Waislamu.

Maelezo ya picha, Mchoro wa kiuhandisi majengo unaoonyesha jinsi eneo jipya la ubatizo linatakavyoonekana "Kila mara ni vizuri sana kuwa na wageni, hija zetu, uzoefu wa kile John (Yohana) na Yesu walichofanya," anasema Rustom Mkhjian, mkurugenzi mkuu wa eneo la ubatizo la Jordan.

"Ninaiita injili ya tano', unavyoangaliwa kwa macho kile unachokisoma katika injiri zote mbili. Kusema kweli unahisi uko katikati ya historia ya dini na imani."



Miongoni mwa vitu vingi anavyovielezea ni mmea asilia wenye nyuki, unaoitwa ganda la nzige, unanikumbusha kwamba katika Biblia- Mtakatifu John akiwa amevalia mavazi ya nyewele za ngamia, akila "nzige na asali ya nyikani".

Eneo la ubatizo, linalofahamikapia kama Bethany zaidi ya Jordan, ni eneo la Urithi la Unesco, ambako kuna magofu ya makanisa ya Waroma na Byzantine, makazi ya watawa na vidimbwi vya ubatizo ni miongoni mwa eneo hilo la nyika.

Yalivumbuliwa katika mwaka 1995 baada ya mkataba wa amani wa Jordan na Israeli.

Kabla ya hapo, pande zote mbili za mto zilikuwa ni eneo lililofungwa la jeshi tangu vita vya mwaka 1967 vya Mashariki ya Kati, ambapo Israeli iliuteka ukingo wa magharibi wa kutoka Jordan na kuutwaa.

Maelezo ya picha, Pango dogo katika kile kinachofahamika kama mlima wa Eliya, ambapo inasemekana kuwa Yohana Mbatizaji aliishi.

"Kuvumbuliwa kwa eneo hili ni moja ya matunda ya amani," Bw Mkhjian anasema. "Fikiria, maeneo makubwa 11 ya migodi yalifunikwa. Ninazungumzia kuhusu maelfu kwa maelfu uwanja ya migodi ilichukuliwa. Si bora kuwa na mamilioni ya mahujaji badala ya migodi?.

Ingawa Wajordan wanashindana na udhibiti wa Waisraeli kuwachukua watalii wanaotembelea mto Jordan, katika miongo miwili iliyopita mapapa wawili wa kikatoliki na viongozi wa kidini wa kanisa kutoka katika maeneo mbali mbali ya duni wametembelea eneo la al-Maghtas.



Watu tajiri na maarufu wamewaleta watoto wao kubatizwa hapa , na mahakama ya ufalme ya Jordan imetuma maji matakatifu kwa ajili ya ubatizo wa watu wa familia ya wafalme wa Uingereza.

Kwa mwaliko wa mamlaka za Jordan Wakristo wa madhehebu mbali mbali wamejenga hapa makanisa mapya, huku mengine yakipangwa kujengwa. Inalifanya eneo hili kuwa moja ya maeneo nadra katika Mashariki ya Kati.

"Inafurahisha moyo," mgeni kutoka Marekani, Sharon ananiambia, akisifu mpango huu wa ujenzi ya familia ya ufalme ya Kiislamu ya Jordan.

"Tunajifunza ni kwa jiasi gano sote tuna mambo yanayofanana, na kwamba serikali ya Jordan inaanzisha yote haya kuipatia kila dini inachohitaji na kukipata hapa katika jengo linaloshirikisha watu wad ini mbali mbali."

Maelezo ya picha, Jengo la kihistoria lenye muundo wa msalaba la ubatizo lililojengwa mahala ambapo inaaminiwa kuwa Yesu alibatizwa, sasa lipo mita 300 (takriban futi 1,000) kutoka kwenye Mto Jordan. Ramani ya eneo jipya la ubatizo kwa lenye ukubwa wa hekari 340-, lililopo karibu na eneo la Unesco, lilizinduliwa mwezi uliopita na Mfalme Abdullah.

Samir Murad, ambaye anaoongoza wakfu ulioanzishwa na serikali ya Jordan kusimamia mradi, anasisistiza kuwa uadilifu wa eneo utaimarishwa.

"Itakuwa ni ujinga na ukosefu wa busara kujaribu kubuni eneo la utalii ambalo lina misingi ya kibiashara na masuala yaliyojaa mada katyika eneo takatifu sana park- ," anasema.

"Tukumbuke kwamba hili ni eneo takatifu zaidi katika Ukristo.

Hapa ni mahala ambapo Yesu alipata wito wake na itakuwa ni makosa sana, iwapo utaliharibu au kukiuka maadili yake kwa njia yoyote ile ."

Maelezo ya picha, Eneo la ubatizo linalofahamika kama Bethany mbali na Jordan linajumisha mfumo wa kukusanya maji

Mipango ya ujenzi mpya inajumuisha kile kinachofahamika kama eneo la malazi na migahawa ya chakula, inayotoa huduma ya vyakula asilia vinavyolimwa Jordan. Nyaya za Intaneti na umeme zitafichwa chini ya ardhi.

Sehemu kubwa yae neo hilo itatunzwa kwa ajili ya kilimo na ndege wa kufugwa ili kulinda mazingira. Msaada wa ujenzi wa bustani unatafutwa kutoka kwa taasisi ya Royal Botanic Gardens iliyopo Kew nchini Uingereza ili kupandwa upya kwa mimea ya iliyotajwa katika Biblia.

Jordha inawaomba wahisani wa kimataifa – zikiwemo serikali na mashirika ya kidini kuchangia garama.

Katika eneo linalokabiliwa na mzozo, ambao kwa sehemu moja inasababishwa na migawanyiko ya kidini, matumaini ni kwamba kwa mradi huo itawaonyesha wengine utamadini wake wa uwazi na maelewano ya mchanganyiko dini tofauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live