Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EAGT wataka Watanzania kujengeana uwezo kiuchumi

A5fb16c61895f85825e623b99649279d EAGT wataka Watanzania kujengeana uwezo kiuchumi

Sun, 1 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KANISA la Evangelist Assembilies of God Tanzania (EAGT) Gethsemane la Kibaha limewataka Watanzania kujengeana uwezo na kubuni miradi ya mbalimbali ikiwamo ya kiuchumi ili kujiongezea kipato, badala ya kutegemea wafadhili.

Katibu wa EAGT Gethsemane la Kibaha, Allen Shayo aliyekuwa mgeni rasmi katika tamasha la kutambulisha Umoja wa Waimbaji Wilaya ya Kibaha lilofanyika katika Kanisa la Church of God of Prophecy Mwendapole Kibaha, alisema jamii inapaswa kuwezeshana kwa kuunda vikundi na kuanzisha miradi itakayotokana na uwezeshanaji wa kiujuzi na kifedha.

“Nawapongeza kwa umoja wenu; haya ndiyo mambo yanayotakiwa watu kuungana na kuanzisha mifuko ya fedha ya kuchangiana hilo ni jambo jema kuliko kusubiri wafadhili wa kuwasaidia,"” alisema Shayo.

Alisema kwa kuwa tayari Tanzania imeingia katika uchumi wa kati, kuungana kutasaidia wananchi kukopesheka ili hatimaye wajasiriamali na wananchi kwa jumla, wawe sifa za kukopeshwa ili waendeleza shughuli zao za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogovidogo.

"Msikae kusubiri wafadhili kwa ajili ya kuwezeshwa; mnaweza kuwezeshana wenyewe kwa wenyewe kwa michango mnayoitoa ambapo mnakopeshana hili jambo zuri na litaleta manufaa kwa mtu mmoja mmoja, taifa na jamii kwa jumla," alisema Shayo.

Kwa mujibu wa Shayo, jamii inapaswa kuwa na uwezo wa kujitegemea kumudu kupata mahitaji muhimu kupitia miradi midogo midogo ya ujasiriamali.

“Tumieni ujuzi wenu mlionao kujikwamua kupitia fedha mnazokopeshana kwenye mfuko wenu ili muweze kujiinua kiuchumi," alisema.

Msoma risala, Dorice Elijah alisema mbali ya shughuli za uimbaji, wana mfuko wa kuweka na kukopa ambao tayari una Sh milioni mbili.

Elijah alisema wanalenga kuwa na chanzo cha mapato ili waendeshe shughuli zao za kila siku ikiwa ni pamoja na kuwa na studio ya kurekodi nyimbo.

Chanzo: habarileo.co.tz