Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dunia itamkumbuka Magufuli kwa ujasiri wake-Shehe Jalala

79563c0628764907abcc218bfbf1ea31.jpeg Dunia itamkumbuka Magufuli kwa ujasiri wake-Shehe Jalala

Tue, 23 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KIONGOZI wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ithnasheriya Tanzania, Shehe Hemed Jalala amesema dunia itamkumbuka Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli kwa ujasiri wake wa kupambana na mabeberu ambao walikuwa wanainyonya nchi.

Akizungumza katika Msikiti wa Ghadir, Dar es Salaam, Shehe Jalala alisema kitendo Rais Magufuli kuwataja wazi mabeberu na kubainisha uovu wao ni cha ujasiri na kinapaswa kuigwa na viongozi wengine.

“Hayati Magufuli alitueleza jambo kubwa na muhimu juu ya mbinu za mabeberu, mbinu za wanyonya, watu wanaotaka siku zote waishi kwa migongo ya Watanzania na migongo ya Waafrika.”

“Afrika tusingeishi katika mazingira ya umasikini na hali tuliyonayo na wala tusinge kuwa na maradhi haya tuliyo nayo yanayotumaliza kila siku kama tungekuwa na watu aina ya Magufuli wanaoponga dhuluma,” alisema.

Shehe Jalala alisema kiongozi huyo pia atakumbukwa kwa kumtanguliza Mungu katika kila jambo na kila hali, kitu kinachowafundisha Watanzania kuwa watu wa swala.

“Wakati mwingine huenda viongozi wa dini tulirudi nyuma, yeye alikuwa mstari wa mbele katika kumuamini Mungu,” alisema.

“Watanzania tutaendelee kukumbuka na kuenzi amani, upendo, mshikamano na umoja aliotuachia, Watanzania kamwe wasikubali kuhatarisha amani, mshikamano na umoja uliokuwa ukipiganiwa na Magufuli.”

“Misingi mikubwa ya nchi ni amani, upendo na umoja, katika kipindi chote cha maisha yake ya uongozi alihakikisha Tanzania inakuwa nchi ya kuigwa katika nyanja hizo.”

“Niwaombe Watanzania kwenye kipindi hiki ambacho ni cha majonzi na huzuni, ni kipindi cha kutafakari, tuzidi kudumisha umoja, mshikamano wetu, tuzidi kuenzi amani ya nchi yetu, tusiyakubali maneno ya mtu yeyote yanayoandikwa kwenye mitandao ya kijamii iwe katika facebook, iwe ni twitter, iwe ni Instagram kwani yanajaribu kuwatikisa Watanzania na kuwatoa katika mstari wao wa umoja, amani na mshikamano," alisema.

Shehe Balala pia aliwataka Watanzania kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi hiki ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kuliletea maendeleo taifa bila ya kuyumbishwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz