Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Shoo awataka Watanzania kuomba toba ya mauaji

Shoo Pic Data Dk Shoo awataka Watanzania kuomba toba ya mauaji

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo amewataka watanzania kuwa na hofu ya Mungu na kuomba toba juu ya mauaji ya kikatili yanayoendelea nchini.

Askofu Shoo ametoa rai hiyo wakati akihubiri kwenye ibada katika usharika wa Moshi Mjini, wakati wa kumuingiza kazini katibu mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa hilo, Zebadiah Moshi pamoja na kuwabariki watheolojia wanne kuwa wachungaji.

Amesema katika kipindi hiki cha kwaresma, ni wakati wa kumlilia Mungu na kuomba toba ili Mungu asiachilie hasira yake.

"Kipindi hiki cha kwaresma tukaone ni wapi tumekwenda kinyume na mapenzi ya Mungu kama mtu binafsi na kama taifa na tumsihi Roho mtakatifu atupe nguvu ya kukaa mbali na dhami na kuyashinda majaribu, tunahitaji toba ya kweli ili hasira ya Mungu isije ikawaka juu yetu" amesema Dk Shoo.

Amesema toka kuanza kwa mwaka huu wa 2022 zimesikika taarifa nyingi za mauaji ya kikatili na umwagaji wa damu jambo ambalo linapaswa kukemewa na kika mmoja kwa nafasi yake.

"Tumeshuhudia kwa wingi sana na tunasikia habari za mauaji na umwagaji damu wa kikatili kabisa na katika mauaji mengi yanayofanyika unasikia watu wamechinjwa kwa kukatwa shingo, tunahitaji toba ya kweli, tumuombe Mungu atusamehe dhambi hii"

"Changamoto za maisha, tamaa za mwili, tamaa za mali, kiburi cha kiroho ni majaribu halisi, tunaweza kuyashinda kwa kumtegemea na kumtii Mungu, tunapaswa kuwa na hofu ya Mungu".

Katibu Mkuu Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa hilo, Zebadiah Moshi ameahidi kufanya kazi hiyo kwa bidii, uadilifu na ujasiri mkubwa, ambapo aliwataka waumini wa kanisa hilo kumuombea ili kuweza kuifanya kazi hiyo kulingana na mapenzi ya Mungu mwenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live