Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dk Mokiwa: Nipo huku mnaotaka kujumuika nami karibuni

67348 Mokiwa+pic

Thu, 18 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jina la Askofu Dk Valentino Mokiwa sio geni masikioni mwa watu hasa waumini wa Kanisa la Anglikana ambalo amelitumikia kwa muda mrefu, na kwa waumini wa Dayosisi ya Dar es Salaam, watamkumbuka zaidi kutokana na mvutano uliojitokeza mwaka 2017.

Chanzo cha mvutano huo uliosababisha mgawanyiko wa waumini wa Anglikana katika dayosisi hiyo, ulitokana na hatua ya aliyekuwa Askofu mkuu wa kanisa hilo, Dk Jacob Chimeledya kuamuru Dk Mokiwa ajiuzulu kwa hiyari yake kutokana na madai ya tuhuma mbalimbali alizokuwa akikabiliwa nazo kwa wakati huo.

Baadhi ya maaskofu akiwamo Elias Chakupewa aliyekuwa Tabora alionesha kutokukubaliana na uamuzi uliofanywa na Chimeledya dhidi ya Dk Mokiwa.

Dk Chimeledya ambaye pia aliwahi kuwa askofu wa Anglikana Jimbo la Mpwapwa, alidai Dk Mokiwa alivunja miiko ya kanisa hilo na kutumia madaraka yake vibaya ikiwamo ubadhirifu wa fedha.Hata hivyo, kwa nyakati tofauti Dk Mokiwa alizikana tuhuma hizo akisema mgogoro wa kanisa hilo umetengenezwa na maadui wake, mwishowe aliondolewa kwenye nafasi hiyo na kutakiwa kutokwenda kwenye kanisa lolote la Anglikana kushiriki au kutoa huduma za kiroho.

Baada ya Dk Mokiwa kuondolewa katika nafasi hiyo, Dk Chimeledya alimtangaza Kasisi Jerome Nampera kukaimu usimamizi wa muda wa shughuli za Dar es Salaam, miezi kadhaa baadae wajumbe wa Sinodi wa dayosisi hiyo walimchagua mchungaji Jackson Sosthenes kuwa askofu wa tano wa dayosisi hiyo akichukua nafasi ya Mokiwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz