Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC aomba viongozi wa dini kusaidia elimu chanjo ya corona

E3dcaa5a7cc3a6e74bdcb4b778f11c54.jpeg DC aomba viongozi wa dini kusaidia elimu chanjo ya corona

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imewaomba viongozi wa dini kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19 na kuelimisha jamii kuhusu chanjo inayoendelea sasa.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Saidi Mtanda alisema hayo akizungumza na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini wilayani hapa .

Mtanda aliwaomba viongozi wa dini kushirikiana na serikali kutoa Elimu kwa jamii ili kulinda nguvu kazi ya taifa.

Alisema kumekuwepo na taarifa potofu juu ya ugonjwa wa Uviko 19 pamoja na chanjo zinazotolewa jambo ambalo Serikali na viongozi wa dini wanaweza kulisimamia ili kueleza ukweli.

Mtanda amesema Corona ipo na tayari Mkoa wa Kilimanjaro umepatiwa dozi 60,000 na kuwaomba viongozi hao kutoa elimu kwa waumini wao kwenda kupatiwa Chanjo hususani wazee.

Amesema wimbi la Sasa la ugonjwa huo ni kali kuliko zilizopita hivyo ni muhimu kila mwananchi akachukua tahadhari ya kujikinga.

Nao baadhi ya Viongozi wa Dini wamepongeza hatua ya serikali katika kuwashirikisha katika kutekeleza majukumu kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.

Chanzo: www.habarileo.co.tz