Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Dodoma atangaza operesheni kuwasaka vibaka

77101 Dodoma+pic

Wed, 25 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma (DC) nchini Tanzania, Patrobas Katambi amesema polisi wameanza operesheni ya kuwasaka vibaka katika maeneo mbalimbali jijini humo.

Akizungumza leo Jumanne Septemba 24, 2019, Katambi ametaja maeneo yaliyokithiri kwa tatizo hilo ni Chang’ombe, mjini na Kisasa.

“Jana tumeanza operesheni maalum ya kuwakamata vibaka na hatumuonei mtu kwa kweli katika kuwakamata,” amesema Katambi

Hata hivyo, amesema wahalifu hao wanatoka katika maeneo mengine ya nchini, vijiwe vya kuvutia bangi.

Kwa upande wake, Diwani wa Chang’ombe, Bakari Fundikira amesema changamoto ya vibaka katika eneo lake ni ya siku nyingi lakini kwa sasa limepungua baada ya kuchukua hatua.

Amesema hatua walizochukua kwa kushirikiana na Polisi zilisaidia kupunguza matukio hayo lakini baada ya kulegeza vibaka wamerejea.

Pia Soma

Advertisement

“Tulikaa kamati ya ulinzi na usalama ya kata. Tukaanzisha operesheni maalum kwa kushirikiana na Polisi,” amesema.

Amesema vibaka hao wamekuwa wakitumia njia tofauti ikiwa ni kutembea na bodaboda na kuwakwapua wanawake wanaopita njiani na wengine wamekuwa wakiingia majumbani.

Mkazi wa Area D, Moses Musa amesema maeneo mengi hivi sasa mara baada ya Serikali kuhamia jijini Dodoma yamekuwa yakikabiliwa na matatizo ya vibaka.

“Hata huku kwetu wiki mbili zilizopita kuna watu wamepigwa mapanga na kunyang’anywa simu na pochi na vibaka wanaotembea na bodaboda,” amesema.

Amesema kabla ya ujio wa Serikali, walikuwa wakianika nguo nje ya nyumba na asubuhi wanazikuta lakini sasa hali haiko hivyo, kwa sababu wanapita vibaka hata mchana kuangalia cha kuiba.

Alipoulizwa kuhusu tatizo la vibaka, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema taarifa za vibaka hao wanazo  na kuwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa.

Amesema kutokana na wanaoporwa kuwalalamikia madereva bodaboda, Muroto amesema wamekuwa wanakamata baadhi ya madereva  bodaboda wanaodaiwa kuhusika kwa ajili ya upelelezi.

Chanzo: mwananchi.co.tz