Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Covid 19 usiwakatishe tamaa ya kuishi, chukueni tahadhari – Mchungaji Mollel

Covid 19 usiwakatishe tamaa ya kuishi, chukueni tahadhari – Mchungaji Mollel

Mon, 13 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Watanzania wametakiwa kutokata tamaa ya maisha kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona kwa sababu utapita.

Mchungaji Baraka Mollel wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Irkiranyi, akiongoza Misa ya Pasaka leo Jumapili Aprili 12, 2020,  amesema  cha msingi na muhimu kwa Watanzania ni kuendelea kuchukua tahadhali dhidi ya virusi vya corona kwa kuvidhibiti badala ya kukata tamaa na kutofanya kazi .

Mchungaji Mollel amesema miaka ya  1,800 ugonjwa kama corona pia uliikumba dunia na kusababisha vifo vya watu wengi lakini ulipita.

Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Ezekiel Lemaso naye amewataka waumini wa kanisa hilo kusali kwa tahadhali na kufuata maelekezo yote yatolewa na wataalamu wa afya na Serikali kwa kuepuka misongamano na kutakasa mikono yao kila mara.

Pia, amewataka waumini kuendelea kufanya Ibada na kumuomba Mungu awaepushe na maradhi hayo.

Chanzo: mwananchi.co.tz