Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Corona ilivyobadili taratibu makanisani

Corona ilivyobadili taratibu makanisani

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mamia ya waumini wa kanisa Katoliki jana Alhamisi Machi 19, 2020  wamejitokeza katika kanisa kuu la Kristu Mfalme jimbo la Moshi kushuhudia kusimikwa Askofu Ludovick Joseph Minde huku taratibu zilizozoeleka katika misa hiyo kutofanyika kutokana na tahadhari ya maambukizi ya virusi vya corona. Askofu Minde ambaye anakuwa Askofu wa nane wa Jimbo Katoliki Moshi, alisimikwa  kuwa askofu wa jimbo hilo akitokea jimbo Katoliki Kahama. Kutokana na tishio la ugonjwa wa corona tahadhari mbalimbali zimechukuliwa ambapo katika milango ya  kuingia katika  kanisa hilo, kuliwekwa maji yenye dawa na sabuni na waumini walipaswa kunawa mikono. Waumini walisisitizwa  kutoshikana mkono na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali ili kuchukua tahadhari. Badala ya utaratibu wa kawaida wa kuwawekea mikono kichwani  mapadri wa jimbo atakalo liongoza baada ya kusimikwa, walipongezana kwa ishara. Wakati wa wakimpongeza kwa kusimikwa, maaskofu wenzake walitoka mbele na  kuinama na kuondoka tofauti na ilivyozoeleka ambapo hupeana mikono. Akizungumza Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Katoliki Katoliki Arusha, Isaac Aman aliwataka wananchi kuacha mzaha na kuhakikisha wanachukua tahadhari dhidi ya corona. "Tuchukue tahadhari zinazostahili dhidi ya ugonjwa wa corona, msifanye mzaha na utani ugonjwa huu ni hatari na watu wanaangamia, tufuate maelekezo yanayotolewa na Serikali kupitia vyombo vya habari na kumuomba Mungu katika hili," amesema  Amani. Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, vyama vya siasa na Serikali.

Chanzo: mwananchi.co.tz