Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chuo chaomba kuruhusiwa kudahili

Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba mkoani Kagera, Desiderius Rwoma amesema Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kadinali Rugambwa (CARUMUCo) kinakufa taratibu baada ya kuzuiwa kudahili wanafunzi licha ya kufuata maelekezo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Desemba 20, 2018 mjini Bukoba wakati akizungumza katika mjadala  wa hatima ya ukuaji wa elimu katika vyuo vikuu vilivyopo Mkoa wa Kagera katika kikao cha kamati ya ushauri wa Mkoa.

Amebainisha kuwa amelazimika kuajiri maprofesa wawili kama sehemu ya masharti lakini hawajapewa jibu na mamlaka iliyowazuia.

Amesema hali hiyo inatishia uhai wa chuo hicho na kwamba kinaweza kufa taratibu huku akiomba waruhusiwe kuendelea na udahili.

Mwenyekiti wa kikao hicho Brigedia Jenerali Marco Gaguti ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera amesema suala hilo litaangaliwa bila kuathiri taratibu zilizopo.

Septemba 25, 2018 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilitangaza kuvifuta vyuo vikuu viwili, kusitisha kutoa mafunzo vyuo vikuu vitano na vyuo vikuu saba vikiwa chini ya uangalizi na kuagiza vyuo hivyo vinavyotakiwa kuwahamisha wanafunzi kutekeleza agizo hilo kabla ya mwaka wa masomo 2018/19 kuanza.

Miongoni wa vyuo vilivyozuiwa kudahili ni CARUMUCo.



Chanzo: mwananchi.co.tz