Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama cha maaskofu chataka haki uchaguzi

A768032ae3f234ef6b92b533ffff9a79.jpeg Chama cha maaskofu chataka haki uchaguzi

Wed, 7 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha Maaskofu na Wachungaji (TPA) kimeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ili haki itendeke.

Kimesema usimamizi wa sheria, kanuni, taratibu na miongozo kuhusu uchaguzi utasababisha vyama vyote kupata haki stahili na hivyo, kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakijitokeza uchaguzi unapowadia na wakati mwingine kukaribia kutishia amani ya nchi.

Rais wa TPA, Askofu Musa Mlawi, alitoa rai hiyo wakati akizungumza na waumini kutoka madhehebu mbalimbali ya dini katika kongamano la kitaifa la maombi lililofanyika jijini Dodoma.

Mlawi alisema Watanzania wanatarajia kuona Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasimamia haki na kufuata sheria, miongozo, kanuni na taratibu za uchjaguzi ili kuepuka malalamiko yanayoanza kujitokeza.

Aliwahakikishia Watanzania kuwa, Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utafanyika mwaka huu utakuwa huru na haki, licha ya kuwapo dosari ndogo ndogo zinazojitokeza.

Alisema chama hicho kinaamini kwa asilimia zote kuwa uchaguzi huo utakuwa wa haki na huru, kutokana na watanzania walio wengi wamekuwa waaminifu kwa kuuombea mbele za Mungu kwa uaminifu.

Kwa mujibu wa Askofu Mlawi, kutokana na upendo wa Watanzania kuombea uchaguzi huu, chama hicho cha maaskofu na wachungaji kinaamini utafanyika kwa amani na taifa litapa viongozi ambao ni chaguo la Mungu.

Aliwataka Watanzania wenye vitambulisho vya kupigia kura, kutimiza haki yao ya kimsingi kwa kujitokeza kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka kwa manufaa ya taifa.

Wakati huo huo: Askofu Mlawi ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John magufuli kwa kuboresha miuondombinu mbalimbali na kuimarisha uhusiano kati ya serikali na viongozi wa dini nchini.

Chanzo: habarileo.co.tz