Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama cha Maaskofu na Wachungaji kumtuza JPM

79b3e22c0d06503146c17bc3e770c305 Chama cha Maaskofu na Wachungaji kumtuza JPM

Thu, 1 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha Maaskofu na Wachungaji Nchini (TPA) kimeandaa tuzo ya heshima ya shukrani kwa Rais John Magufuli wakati wa Kongamano la Maombi la Kitaifa la Kuombea Uchaguzi Mkuu litakalofanyika leo katika viwanja vya Jamhuri jijini hapa.

Rais wa TPA, Askofu Musa Mlawi, aliyasema hayo jijini hapa wakati akizungumzia mpango huo wa kumpatia Rais Magufuli tuzo hiyo kama sehemu ya kutambua kazi kubwa aliyoifanya katika muhula wa kwanza wa miaka mitano ya uongozi wake.

Mlawi alisema Rais Magufuli ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi atapewa tuzo hiyo kwenye kongamano hilo la maombi ya kitaifa kuombea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Tuzo hiyo wataitoa kwa Rais Magufuli kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake wa miaka mitano.

“Mambo mengi aliyofanya Rais Magufuli, kwa uchache tu ni pamoja na kuboresha miundombinu pamoja na kuimarisha uhusiano kati ya serikali na viongozi wa dini nchini,” alisema Askofu Mlawi.

Pia, alisema pamoja na kutoa tuzo hiyo chama cha maaskofu na wachungaji nchini kwa kushirikina na viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali watakuwa na Kongamano la kuombea Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

“Kongamano hilo la maombi litajumuisha watu mbalimbali na kupitia maombi hayo yanakwenda kufungua baraka katika uchaguzi mkuu 2020, ili upite katika hali ya utulivu na amani kubwa,” alisema.

Aidha, aliwataka Watanzania kuhakikisha wanajitokeza kupiga kura na kumchagua kiongozi bora atakayeongoza nchi kwa miaka mingine mitano.

Vilevile, aliwataka wagombea wa nafasi zote za kisiasa urais, ubunge na udiwani kutumia mikutano ya kampeni kunadi sera za vyama vyao na kuacha kutumia lugha za matusi kuchafuana.

Chanzo: habarileo.co.tz