Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bwana harusi aliyefariki kuzikwa kesho Marangu

34302 Pic+harusi Tanzania Web Photo

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mazishi ya bwana harusi, Heaven Makupa aliyefariki muda mfupi kabla ya kufunga ndoa yanatarajiwa kufanyika Jumatano, Marangu mkoani Kilimanjaro.

Makupa alifariki Jumamosi Desemba 29 jioni baada ya kuugua ghafla akiwa Kanisa la Nabii wa Utukufu wa Bwana jijini Arusha muda mfupi kabla ya kufunga ndoa na Jane Kimaro.

Tukio hilo lilitokea wakati bibi harusi akiingia kanisani huku tayari maandalizi yote muhimu yakiwa yamekamilika.

Baada ya ndoa hiyo kufungwa, ilitarajiwa kufuatiwa na sherehe iliyokuwa ifanyike katika ukumbi wa Sariko Olasiti Garden.

Akizungumza na Mwananchi jana, ndugu wa marehemu, Richard Makupa alisema maziko yatafanyika Jumatano kama ndugu walivyokubaliana. “Muda huu nipo barabarani naelekea huko,” alisema.

Alisema msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Kwamrombo nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Akizungumzia msiba huo, Nabii wa Utukufu wa Bwana, Peter Alayce alisema Makupa alifariki dunia baada ya kupandwa na shinikizo la damu (BP) ghafla.

“Kabla ya ndoa kufungwa bwana harusi presha ilikuwa juu sana ndipo alikimbizwa Hospitali ya St Elizabeth,” alisema nabii huyo.

Alisema baada ya kufikishwa hospitalini alifariki.

“Baada ya kama nusu saa hivi, tulipata taarifa kuwa tayari ameshafariki dunia,” alisema.

Kiongozi huyo alipoulizwa kuhusu hali ya bibi harusi, alisema hayupo katika hali nzuri na hawezi kulizungumzia tukio hilo. “Yupo kwenye wakati mgumu sana, hawezi kusema chochote, tumuache tu,” alisisitiza.

Soma zaidi: Bwana harusi afariki dunia akisubiri kufunga ndoa kanisani



Chanzo: mwananchi.co.tz