Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bundi atua Kanisani kwa Kakobe, Mchungaji afurushwa

Operanews1690557583874 Bundi atua Kanisani kwa Kakobe, Mchungaji afurushwa

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bundi ametua rasmi kwenye huduma ya Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship jimbo la Dodoma baada ya uongozi wa jimbo kudaiwa kuvamia kanisa linalosimamiwa na Mchungaji Benson Rutta wilayani Kondoa mkoani humo na kujitwalia mali za kanisa hilo bila kumshirikisha. Anaripoti Danson Kaikage, Dodoma … (endelea).

Kanisa hilo ni moja ya makanisa 400 yanayosimamiwa na Askofu Zacharia Kakobe ambaye ndiye mwanzilishi na Msimazi Mkuu wa makanisa ya Full Gospel Bible Fellowship Church yenye maelfu ya waumini jijini Dar-Es-Salaam na Tanzania nzima.

Aidha, akizungumzia kuhusu mgogoro huo, Mchungaji Benson Rutta alisema mtafaruku ndani ya kanisa hilo, unatoke wakati viongozi mbalimbali wakiimba na kuhimiza amani.

Alifafanua kuwa katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship katika jimbo Dodoma uongozi huwapora wachungaji nafasi zao na kutumia lugha chafu kwa wahumini wa kanisa hilo.

Mchungaji Rutta anaeleza kuwa amekuwa mchungaji wa kanisa hilo zaidi ya miaka 20 lakini amejikuta katika wakati mgumu baada ya uongozi wa jimbo la Dodoma kuvamia kanisa alilokuwa akilichunga huko Kondoa kwa kuvunja milango na kudaiwa kuwa yeye hastahili kuwa mchungaji wa kanisa hilo tena.

“Nimekuwa mchungaji wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship tangu nikiwa kijana na kuacha kazi yangu nikiwa shirika la posta na simu na kujiunga na huduma ya Askofu Zacharia Kakobe.

“Nilianza kazi ya Mungu hapo Kondoa pakiwepo na ugumu wa kutisha kutokana na imani ya wanakondoa lakini nilisimama huku nikiamini kuwa mwajiri wangu ni Roho Mtakatifu.

“Kwa kuamini hivyo nilijitolea kwa hali na mali kwa kuuza hata baadhi ya viwanja na mashamba kwa lengo la kuifanikisha kazi ya Mungu lakini cha kushangaza uongozi wa mkoa kwa kushirikiana na uongozi taifa wamevizia sipo wameingia kanisani kwa kuvunja milango na kuchukua mali za kanisa huku wakizuia mimi na familia yangu kutokuchukua kitu chochote” ameeleza mchungaji Rutta.

Mchungaji Rutta anaeleza kuwa mgogoro huo unatokana na uongozi wa mkoa kuwa na fikra potofu juu ya misimamo yake ya kujiendeleza kimasomo na kufikia hatua ya kupata elimu ya juu ya PhD.

Amesema Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lina misingi ya kuwataka viongozi kujiendeleza kielimu lakini pia kutokubaliana na mchungaji wa kanisa hilo kutokuwa na huduma inayomtambulisha nje ya kanisa hilo.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa hilo Jimbo la Dodoma, Neema Mduma alipoulizwa juu ya kuwepo kwa mtafaruku huo amesema kuwa yeye siyo msemaji na anachoweza kusema ni kuwa mchungaji Rutta alifungua huduma ndani ya kanisa hilo.

“Mimi siyo msemaji wa kanisa nadhani wasemaji wa kanisa unawajua, mimi natumika ninapotumwa kutumika, ninaongoza ninapotakiwa kuongoza nikianza kusema nitajikuta nasema na mengine ya makao makuu hivyo mimi siyo msemaji ila kwa ufupi Mchungaji Rutta hatujamfukuza bali amejifukuza mwenyewe kwa kuanzisha huduma ya Glory to God ndani ya kanisa la FGBF,” ameeleza Askofu wa Jimbo la Dodoma.

Alipoulizwa juu ya yeye kutumia lugha chafu kwa waumini wake alisema “yaishie hapo hapo sitaki kusikia, ishia hapo hapo,” akakata simu.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa kanisa hilo, Nathani Meshaki alipoulizwa juu ya kuwepo kwa mpasuko huo ndani ya kanisa hakutaka kufafanua jambo lolote na badala yake alisema kuwa “Hayo yameisha isha, yameisha isha”.

Hata hivyo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi zaidi juu ya jambo hilo alisema mambo hayo yameshandikwa sana kwenye vyombo vya habari hivyo hakuna jibu kipya tena na alikata simu bila kufafanua jambo lolote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live