Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bavicha waomba mambo matatu kanisani, wamtaja Lissu

Mon, 10 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Viongozi na wajumbe wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) leo asubuhi Jumapili Septemba 9, 2018 wameshiriki misa ya shukrani, kumshukuru Mungu kwa mambo makubwa matatu.

Miongoni mwa mambo hayo ni kumshukuru Mungu kwa kumponya na kumuondoa katika tundu la kifo  Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu ambaye Septemba 7, 2017 alishambuliwa kwa risasi nje ya nyumba yake mjini Dodoma, hadi sasa anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji.

Akizungumza na MCL Digital leo, Katibu Mkuu wa Bavicha Julius Mwita amesema waliomba misa hiyo ya shukrani katika Kanisa la St Peter jijini Dar es Salaam.

“Misa ilianza saa moja asubuhi na kumalizika saa tatu, tulikuwa takribani watu 70 pamoja na waumini wengine,” amesema Mwita.

“Jambo la kwanza katika maombi yetu yalikuwa kumuomba Mungu amponye Lissu katika tundu la kifo maana aliweza kutoka hai na mpaka sasa yupo hai licha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30.”

Amesema jambo la pili wamemuomba Mungu amponye mbunge huyo wa Singida Mashariki ili arudi nchini na kuendelea na harakati za kudai demokrasia.

“Tatu, tumemuomba Mungu juu ya utengamano wa Taifa maana kwa sasa Taifa limekuwa likijigawa kwa misingi ya kiitikadi.

“Sisi tuna amini Taifa linajengwa kwa misingi ya mshikamano, umoja, upendo na amani. Na hilo linadhihirika kutokana na kauli na matendo ya baadhi ya viongozi wetu, tunataka viongozi hawa warudi katika misingi tuliyoizoea.”

Chanzo: mwananchi.co.tz