Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bakwata yazindua kampeni za kwenda hijja 2019

Wed, 6 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) limezindua kampeni ya maandalizi ya hija mwaka 2019 yanayolenga kuhamasisha waumini kujiandaa mapema na ibada ya hijja.

Kampeni hiyo imezinduliwa rasmi leo Jumanne Machi 5, 2019 na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Bakwata, Sheikh Hamid Jongo.

Sheikh Jongo amezitaka taasisi hizo kutokuweka mbele maslahi binafsi bali waangalie huduma wanazozitoa kwa mahujaji ili mahujaji hao wakafanikishe moja ya nguzo tano za Kiislamu.

Naye Mratibu wa hijja upande wa Tanzania Bara, Sheikh Mussa Hemed amesema  kampeni hiyo itakuwa na vikundi ambavyo vitasafiri maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha Waislamu kote nchini kuhusu ibada ya hijja.

Mbali na uzinduzi huo Bakwata pia wametangaza taasisi 17 ambazo zitasafirisha mahujaji kwenda nchini Saud Arabia itakapofanyika ibada hiyo.

Sheikh Hemed amezitaka taasisi hizo kukamilisha taratibu zote kwa wakati ili kuondoa dosari ambazo hujitokeza, dosari ambazo zinapelekea baadhi ya mahujaji kushindwa kwenda kutekeleza ibada hiyo inayofanyika kila mwaka.

“Ikitokea taasisi imeshindwa kukamilisha taratibu hizo kwa wakati itaondolewa katika orodha ya wasafirishaji na mwisho wa kukamilisha taratibu hizo ni Aprili 10, 2019,” amesema.

Mratibu msaidizi Idara ya Uhamiaji, Godfrey Silvanas ameliomba baraza hilo kukamilisha taratibu mapema hasa katika suala la hati za kusafiria.

“Tunashukuru kwa ushirikiano, lakini idara inaomba taratibu zote zikamilishwe ikiwemo hati za kusafiria za kielektroniki lakini pia tunaomba tupatiwe idadi ya taasisi zote zitakazosafirisha mahujaji,” amesema.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz