Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bakwata waitisha maandamano Kilimanjaro

Bakwata Picnmm Bakwata waitisha maandamano Kilimanjaro

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Baraza kuu la Waisilamu Tanzania (Bakwata) mkoani Kilimanjaro limeitisha maandamano kwa ajilu ya kupinga vitendo vya ukatili nchini na kuwataka waumini wa dini hiyo kujitokeza kushiriki.

Alipoulizwa kuhusu maandamano hayo, Kamanda wa Polisi mkoa huo, Simon Maigwa amesema ni kweli maandamano hayo yamepewa kibali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 4, Katibu wa Bakwata mkoani hapa, Awadhi Lema, amesema maandamano hayo yatafanyika Aprili 8 mwaka huu.

Lema amesema lengo ya maandamano hayo ni kupaza Sauti kupiga vitendo hivyo ambavyo vinaonekana kuongeza siku hadi siku jambo ambalo linahatarisha kwenye jamii kama litafumbiwa macho.

"Ni kweli tutafanya maandamano kupiga vitendo vya ukatili ili Jamii ya Kitanzania ibaki salama na yenye afya," amesema Lema.

Maandamano hayo yataanzia saa tatu asubuhi ofisi za Bakwata Mkoa hadi viwanja vya Mashujaa Manispaa na kupokelewa na Katibu wa Bakwata Taifa, Nuhu Mruma

Naye Sheikh wa mkoa huo, Shaabani Mlewa, ameomba Waumini kujitokeza kwa wingi siku hiyo.

Chanzo: mwanachidigital