Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bakwata waagiza wanaofungisha ndoa kuwa na leseni halali

Cfab42656403c6c9866174672e1cb24c Bakwata waagiza wanaofungisha ndoa kuwa na leseni halali

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Dodoma limeagiza wale wote wanaofungisha ndoa za kiislamu kuhakikisha wanakuwa na vyeti halisi vya ndoa na leseni maalumu inayotambuliwa na baraza hilo.

Angalizo hilo limetolewa na Katibu wa Bakwata Wilaya ya Dodoma, Ahmed Msuri alipokuwa akizungumza na mashehe, maimamu na walimu wa madrasa kutoka kata za jiji hilo kwenye kikao cha utendaji kilichofanyika kwa ajili ya uchangiaji wa Mfuko Maalumu wa Shehe Mkuu na Mufti wa Tanzania ambao utasaidia makundi maalumu yenye uhitaji.

Katibu huyo alisema hivi sasa kumekuwepo na ufungishaji wa ndoa za Kiislamu holela zisizo halali ambazo hufanyika mitaani huku wakitumia vyeti bandia ambavyo havitambuliwi na baraza hilo.

Alisema hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa migogoro mingi kwenye ndoa isiyokuwa na tija, ambazo zimeshindikana hata kuzitatua kutokana na wengi wao kugundulika kuwa na vyeti feki vya ndoa.

"Lengo la angalizo hili viongozi mliohudhuria kikao hiki mashehe, maimamu na walimu, ni kuwatambua wanaofungisha ndoa hizo kweli wana vibali halali na wapo kisheria na sio vinginevyo, tunahitaji kuheshimu msingi wa dini ya kiislamu tuliyoachiwa na Mtume wetu Muhamad(S.A.W),"alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania Wilaya ya Dodoma, Bashiru Husseni amewataka mashehe na maimamu kujenga ofisi zao kwenye kata ili ziweze kutumika kwa kuondoa kasoro zinazojitokeza ikiwemo hao walimu wanaofungisha ndoa kwa kutumia vyeti feki.

Alisema ofisi hizo zikiwepo wale wote watakaohitaji kufunga ndoa zao watakuwa wakiwafuata ili wapatiwe huduma hiyo muhimu ya kufungishwa, pia wataweza kutatua migogoro kwa njia ya ufanisi zaidi.

Alisema moja ya majukumu yao ni kuhakikisha mashehe wote wa kata wanakuwa na ofisi ili kuleta ufanisi wa katika kazi zao ambapo zitawasaidia pia kuondokana na kufanya kazi zao kwa mazoea.

Chanzo: www.habarileo.co.tz