Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bakwata kusajili misikiti,madrasa zote Tanzania

52278 Pic+bakwata

Mon, 15 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata), limezindua mpango mpya wa vyeti vya ndoa, usajili wa madrasa na walimu, misikiti na utoaji wa vitambulisho kwa wafungishaji ndoa.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumapili Aprili 14, 2019 katika viwanja vya Shule ya  Sekondari ya ya Kiislamu ya Al- Haramain iliyopo Kariakoo wilayani Ilala, Dar es Salaam na ulihudhuriwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir.

Mjumbe Baraza la Ulamaa, Sheikh Hassan Chizenga amesema hatua ya mpango huo imeazimiwa na kikao cha baraza hilo kilichokutana kwa nyakati tofauti chini ya mwenyekiti wake, Sheikh Zubeir.

Sheikh Chizenga amesema kutokana na mpango huo, vyeti vya sasa vya ndoa vitakuwa vimeboreshwa na ndoa itakayofungwa taarifa zake, zitatunzwa katika kanzi data maalumu kupitia namba ya cheti.

“Kupitia namba ya cheti, tutajua kila kitu kuhusiana na ndoa za kiislamu zilizofungwa na idadi yake. Naweza kusema ni cheti bora kwa ndoa za kiislamu, naomba taasisi za Serikali, mabalozi wakipokee kwa mikono miwili pindi wahusika watakapokiwakilisha,” amesema Sheikh Chizenga.

Kuhusu misikiti Sheikh Chizenga, amesema lengo la kuisajili ni kutaka kujua idadi yake kwa nchi nzima ili litapokea tatizo Bakwata ijue namna ya kulitatua kwa kuwa wana taarifa za msikiti husika.

“Hatuna nia ya kuchukua misikiti, bali tunataka kujua idadi na taarifa zao ili linapotokea tatizo inakuwa rahisi kujua njia ya kukabiliana nalo,” amesema Sheikh Chizenga.

Mufti Mkuu, Sheikh Zubeir amesema “Ni jambo kubwa kwa Waislam na Watanzania kwa Bakwata kuwa na vyeti vya ndoa vya kisasa na vilivyoboreshwa katika utaalamu wa hali ya juu.

Awali, Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alitoa wito kwa madrasa na taasisi nyingine za kiislamu za mkoa kujipanga na kujitokeza kujisajili katika mpango huo wenye manufaa makubwa.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz