Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bakwata kufanya dua kuombea mvua

48027 Bakwatapic

Fri, 22 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limeandaa dua maalum ya kuombea mvua itakayofanyika Machi 24, 2019 katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Machi 22, 2019 katibu wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Hassan Chizenga amesema duwa hiyo itaanza leo Ijumaa kwa dua maalum kabla ya kufuatiwa na dua ya kitaifa.

"Leo wakati wa swala ya Ijumaa itaswaliwa dua maalum (kunuti) kwa ajili ya kuomba mvua isiyokuwa na madhara na kufuatia na dua itakayofanyika kitaifa siku ya Jumapili katika viwanja vya mnazi mmoja," amesema Shekh Chizenga.

Amesema dua hiyo ni kutokana na sehemu nyingine kupata mvua zenye maafa na nyingine kukosekana ambapo Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir ameagiza kufanyika kwa dua maalum kwa ajili ya kuomba kupata mvua isiyo na madhara.

"Kutokana na baadhi ya maeneo mengine kukosa mvua tunaomba viongozi na taasisi zote kushiriki katika jambo hili ambalo ni muhimu kwa Taifa ili kuweza kupata mvua,’’ amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz