Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Bado niko hai' Papa Francis atania wakati alipotoka hospitalini

'Bado Niko Hai' Papa Francis Atania Wakati Alipotoka Hospitalini 'Bado niko hai' Papa Francis atania wakati alipotoka hospitalini

Sat, 1 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Papa Francis ametania kuwa "bado yuko hai" alipokuwa akiondoka hospitalini mjini Roma baada ya kukaa kwa siku tatu.

Alilazwa katika Hospitali ya Gemelli katikati ya wiki akiwa na matatizo ya kupumua.

Vatican ilitoa taarifa kuwa atatoka leo Jumamosi, kulingana na matokeo ya vipimo.

"Sikuwa na hofu, bado niko hai," papa huyo mwenye umri wa miaka 86 aliwaambia waandishi wa habari na waombezi wa heri nje ya hospitali kabla ya kuruhusiwa kuondoka hospitali.

Alionekana akitabasamu na kupunga mkono kutoka kwenye gari, kabla ya kutoka nje kuzungumza na umati. Kisha akaelekea Vatican.

Chanzo: Bbc