Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BAKWATA yaja na mambo tisa kukabiliana na ndoa za utotoni

61524 Bakwatapic

Thu, 6 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) limetoa maazimio tisa kumaliza tatizo la ndoa za utotoni na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto ili kulinda haki zao.

Maazimio hayo yametajwa wakati wa uwasilishwaji wa kampeni ya World Vision Tanzania (WVT) jijini Tanga ambayo ulihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela.

Baada ya kuzinduliwa kampeni hiyo, RC Shigela alisema kuwa azimio hilo litaondoa utata wowote uliokuwepo awali, kuhusu dini ya kiislamu na haki za watoto.

Shigela amesema Serikali itatoa ushirikiano katika kampeni hiyo na kuwashauri viongozi wa kiislamu kusambaza elimu kuhusu haki za watoto wa kike, hadi ngazi ya chini ambapo tatizo lipo.

Akisoma azimio hilo Katibu wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Juma alisisitiza kuwa baraza hilo litatoa sapoti kulinda haki za mtoto wa kike na kusisitiza pia wazazi wana jukumu katika kulinda haki hizo za watoto wa kike.

Azimio hilo limejikita katika mambo kadhaa ikiwemo, dini ya kiislam inatambua ndoa kama nguzo muhimu katika ustawi wa binadamu.

Pia Soma

Pili azimio hilo linahimiza  dini ya kiislamu inatambua ndoa ambayo imefanyika kwa makubaliano na watu wawili wa pande mbili kwa mujibu wa dini, na tatu ni kwamba uislamu haujaweka umri wa msichana kuolewa ila anatakiwa awe na afya njema na awe tayari kisaikolojia, kimaumbile na kikanuni za ndoa.

Aidha azimio hilo pia limetaja jambo la nne kuwa wazazi wamepewa mamlaka ya kuwaoza mabinti zao kama wamekubaliana na vigezo vya dini kulingana na kanuni na miongozo ya kiislamu.

Pia azimio limetaja jambo la tano kwamba msichana ambaye anahisi haki zake hazijalindwa ana haki ya kwenda kwa Kadhi na kuomba kuvunjwa ndoa na sita  mtoto ana haki ya kulinda haki zake za utoto kama ilivyo kwa mtoto wa kiume.

Shekih Juma amesema kuwa jambo la saba, linajikita katika kutambua ndoa kama mkataba siriazi unaohitaji kila anayeuingia awe na uelewa wa kutosha wa nini anafanya na wote wanaooana lazima wafanye hivyo kwa ruhusa ya kisheria.

 

Jambo la tisa linasisita uislamu unaelekeza kila mtoto kupewa elimu bila ubaguzi kulingana na maelekezo ya Mtume Mohammad (S.A.W)

 

Akizungumza katika tukio hilo Mkurugenzi wa mradi huo wa World Vision Dk Kasilima Yosh alisema vita ya kumaliza ndoa na mimba za utotoni haikuwa jukumu la taasisi moja bali la Watanzania wote.

 

Tumeshirikiana na Bakwata tangu mwaka 2017 kwa sababu tunaamini katika nguvu ya viongozi wa dini na taasisi kumaliza tatizo hili la ndoa za utotoni, alisema Dk Yosh, huku akiwataka viongozi wote wa deini kuunga mkono kampeni hiyo

Chanzo: mwananchi.co.tz