Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ayub Savula abatizwa Mto Jordan alikobatizwa Yesu

KAKAMEGA ERWWF.png Ayub Savula abatizwa Mto Jordan alikobatizwa Yesu

Mon, 30 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Democratic Action Party of Kenya (DAP-K) kimetangaza kuwa naibu kiongozi wake Ayub Savula ambaye ni naibu gavana wa kaunti ya Kakamega alibatizwa Jumamosi katika Mto Jordan.

Mto Yordani, kama ilivyorekodiwa katika Biblia ya Agano Jipya, ndipo Yesu alipobatizwa pia na Yohana Mbatizaji, ambaye baadaye alimtaja kuwa “Mwana wa Mungu.”

Naibu Gavana wa Kakamega, kulingana na DAP-K, kwa sasa yuko katika ziara ya Israeli kwa misheni ya kujiufnza pamoja na wenzake kutoka kaunti nyingine.

“Naibu kiongozi wetu wa chama DAP-K na naibu gavana wa Kakamega @SavulaHon alibatizwa leo katika Mto Yordani, Israeli, ambapo Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji.

Savula pamoja na Manaibu Gavana wenzake wako nchini Israel kwa ajili ya kujifunza katika kuboresha mamlaka yao na kuimarisha ugatuzi,” chama hicho kiliripoti kupitia ukurasa wao rasmi wa Twitter.

Savula ambaye awali alikuwa na azima ya kuwania kama gavana wa Kakamega kupitia chama hicho aliteuliwa kuwania kama naibu gavana wa Fernandes Barasa wa ODM baada ya vyama hivyo viwili kuungana chini ya mwavuli wa Azimio la Umoja.

Hata hivyo, baada ya tikiti yao ya Barasa- Savula kuibuka washindi dhidi ya mpinzani wao mkuu, Cleophas Malala, Savula alionekana kuanzisha vurugu katika kaunti akitaka kutotambuliwa kama naibu gavana bali gavana mwenza.

Tofauti zao zilitishia kulemaza utendakazi wake na Barasa lakini juhudi za vyama husika ziliyamaliza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live