Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu awataka Wakristo kuwa na roho ya kusamehe

53157 Pic+askofu

Fri, 19 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakristo wametakiwa kuwa na roho ya kusamehe kama ilivyokuwa kwa Yesu wakati wa kuteswa hadi kuuwawa.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Aprili 19, 2019 na Askofu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam, Jackson Sosthenes wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu katika kanisa la Mtakatifu Albano jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Yesu.

Amesema neno la msamaha katika maisha ni jambo la muhimu kwani ni vigumu binadamu kutokwazana.

"Ili uwe na amani na kufanikiwa jambo muhimu ni kuwa na roho ya msamaha kama alivyofanya Yesu kwa wale waliomsulubisha," amesema Askofu Sosthenes.

Amesema ni muhimu kufika sehemu kutokuwa na roho ya kisasi na kuwatangazia neno la msamaha wale waliokuumiza.

"Katika maisha wanaokuumiza ni wengi kuliko wanaokutia moyo inabidi kufika mahali na kuwatangazia msamaha wale wanaokuumiza," amesema.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Mtakatifu Albano, John Mlekano amesema katika jamii tunapaswa kuwa wavumilivu na kutohukumu watu kimakosa.

"Katika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Yesu tunatakiwa kuwa wavumilivu katika changamoto mbalimbali na kuangalia ni wapi tulipohukumu kimakosa," amesema  mchungaji Mlekano.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz