Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu atoa ya moyoni kauli ya Papa Francis kuhusu mashoga

Mwamakula Ms 2 1.jpeg Askofu atoa ya moyoni kauli ya Papa Francis kuhusu mashoga

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

1. Kanisa la Yerusalemu lillitaka pia Kanisa la Antiokia likubali tohara, na Antiokia lilikaza uzi. Nusura Kanisa ligawanyike mapande mawili.

Lakini hekima ya Askofu Mkuu wa Yerusalemu (Papa) au Mtume Yakobo, ilisaidia Kanisa libaki moja kupitia Mtaguso Mkuu (Sinodi Kuu) wa Kwanza ya Kanisa (soma Matendo ya Mitume 15:1-35).

2. Mtume Yohana Marko aliasi kazi ya Injili kwa sababu ya ubinafsi. Mtume Paulo yeye hakuwa tayari kuendelea na mtu aliyeasi Injili na hivyo akataka atengwe kabisa katika utumishi.

Paulo alisisitiza matendo mema na ushuhuda ambao unaonekana kama kigezo cha kuendelea katika huduma, lakini Barnaba alitaka kuijaribu neema kwa matendo hivyo akasisitiza Yohana Marko aendelee kuwa sehemu ya huduma yao.

Lakini hakukuwa na Sinodi ya kusuluhisha kwa hiyo wakatengana (Matendo ya Mitume 15:36-41). Mpasuko ule ndio uliozaa Kanisa la Cyprus na Kanisa la Antiokia (yote haya baadaye yakawa sehemu ya Orthodox Catholic Church).

3. Toka mwaka 500 hadi 1054 Kanisa Katholiko lilikuwa katika mgogoro mzito juu ya kipengere kimoja katika Imani ya Nikea. Kipengere hicho kitheologia kinaitwa the Filoque Controversy, ni kipengere ambacho Kanisa la Rumi lilikiongeza katika Imani ya Nikea. Kipengere hicho ni kile kinachosema kuhusu Roho Mtakatifu atokaye "kwa Baba na Mwana" wakati awali kulikuwa ni "atokaye kwa Baba"! Wagiriki walilaumu Kanisa la Rumi kwa kuasi Ukiri huo, hapo ndio Kanisa lilipasuka rasmi mapande mawili mwaka 1054.

4. Kinachoendelea ndani ya Roman Catholic Church kuhusu kauli ya Papa Francis na kauli za baadhi ya Maaskofu wa Kanisa hilo kutoka Afrika ikiwemo Tanzania na kwingineko kuhusu mjadala wa kutoa baraka kwa mashoga na pia wasagaji ni sehemu ya changamoto ambazo husaidia Kanisa liwe imara zaidi kuliko jana.

5. Kwa muono wetu, Papa Francis hajaukubali ushoga, lakini alikuwa anatafakari huduma ya Kichungaji kwa mashoga - Kanisa haliwachukii waovu na pia haliwatii moyo kuendelea na huo uovu wao. Je, mtu muovu anapongia ndani ya malango ya Kanisa ni nini wajibu wetu? Hiyo, inaweza kuwa ndio tafakuri ya Papa Francis!

6. Maaskofu wengine hawawachukii waovu, ila wanawaza nini madhara ya waovu kuikaribia milango ya Kanisa kirahisi bila ya kuonyesha kuwa wanakuja kutubu?

7. Misimamo yote miwili haikinzani ingawa pia imetengwa na Daraja la Kiteputepu au bovu! Na mtu akivuka bila tahadhari katika daraja hilo na yeye anaweza kutumbukia.

8. Tusikilize, tutafakari, tusihamaki na wala pia tusihukumu. Tuwe makini kusikia tafsiri zenye lengo la kulichafua au kuligawa Kanisa. Kanisa likigawanyika wao wataandika kwa herufi kuu na kupata habari za kusema.

Sisi Askofu Mwamakula, tunapenda kuwatia moyo waumini na hasa wa Roman Catholic Church (RC) walioko Tanzania ili kuendelea kusimamia misingi ya imani iliyo katika Kristo.

Waendelee kusali na kuwaombea viongozi wao bila kijiingiza katika mijadala ya kufedhehesha kama wanavyofanya watu wasiokuwa Wakristo kwa lengo la kuiteteresha imani yetu.

Hakuna kinyonge cho chote kitakachoingia ndani ya Kanisa na kuliangusha. Kanisa hili la Kristo limejengwa katika msingi imara ambao ndio 'mwamba' au 'petra' ambaye ndiye Kristo mwenyewe.

Usilionee haya wala kinyaa Kanisa kwa sababu ya mawimbi yanayolikumba kwani yanaliimarisha zaidi. Ushoga kamwe hauwezi kulitikisa Kanisa. Tulipewa sakramenti ambazo kamwe haziwezi kutenguliwa na udhaifu wetu, viongozi wetu au hata hila za adui wa Kanisa aliyeshindwa Golgotha miaka 2000 iliyopita!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate! Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live