Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu ataka ulipaji kodi uzungumzwe kwenye ibada

65864 Pic+askofu

Mon, 8 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Askofu wa Kanisa la Highway of Holiness Cathedral (HHC) la jijini Mwanza, Eugene Murisa amewataka viongozi wa dini Tanzania kuwahamasisha waumini wao kulipa kodi ili kuiwezesha Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo.

Akizungumza katika Ibada maalumu ya kuliombea Taifa na utekelezaji wa bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2019/20 ya Sh33.1 trilioni, Askofu Murisa amesema uhamasishaji wa kodi uwe ni miongoni mwa mafundisho muhimu wakati wa ibada na mikusanyiko ya kiimani kwenye makanisa na misikiti.

“Viongozi wa dini tuna nafasi ya kuhakikisha Serikali inapata mapato ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuwahamasisha waumini wetu wanaotumaini  kutimiza wajibu wa kulipa kodi,” amesema Askofu Murisa

Amewataka viongozi na watumishi wa umma wenye dhamana ya kukusanya kodi na kupanga matumizi kutimiza wajibu wao kwa uaminifu na weledi ili kutowakatisha tamaa walipa kodi.

Mmoja wa waumini waliohudhuria ibada hiyo, John Senga aliunga mkono kauli ya Askofu Murisa kuhusu weledi na uaminifu miongoni mwa watumishi wa umma wakati wa kukusanya kodi, kupanga matumizi na utekelezaji wa miradi.

Chanzo: mwananchi.co.tz