Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu ataka mashoga wasitengwe, wasaidiwe

26451 ASKOFU+PIC TanzaniaWeb

Sun, 11 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba mkoani Kagera, Desiderius Rwoma amekemea vitendo vya ushoga na kutaka wanaofanya dhambi hiyo wasitengwe na kubaguliwa badala yake wasaidiwe na kuonyeshwa ubaya wa wanachofanya.

Amesema kumvumilia mkosefu yeyote haina maana ya kumuunga mkono na kuwa ushoga ni dhambi na laana na watu wenye tabia hiyo wanahitaji msaada wa matibabu na huduma za kisaikolojia.

Katika mahubiri yake leo katika siku ya wanaume wa Jimbo Katoliki kwenye kanisa la Bikra Maria Mama wa Huruma, Askofu Rwoma ametaka uwepo wa sheria za kudhibiti vitendo vya ushoga.

Alipoulizwa na Mwananchi mbona katika mahuburi alionyesha wasiwasi wa kauli iliyotolewa na kiongozi mmpja wa Serikali kuwa 'Tanzania ni Hekalu la Mungu' alisema kwa kuwa nchi haina dini kwa watu wenye nia mbaya kauli hiyo inaweza kuwachanganya.

Alisema lengo la kauli hiyo ilikuwa ni kutaka kuonyesha vitendo vya ushoga ni aibu na havikubaliki kwa Watanzania na kuwa wanaume wana nguvu kubwa ya kufanikisha vita dhidi ya uovu huo.

Chanzo: mwananchi.co.tz