Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu ataja ushindi wa Simba ibada ya Krismasi

Wed, 26 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Unaweza kusema Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (Dodoma), Dk Dickson Chilongani amepeleka ushindi wa klabu ya Simba dhidi ya Nkana ya Zambia kanisani.

Hiyo ni kutokana na askofu huyo kuipongeza timu hiyo kwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1 na kuwafanya waumini kulipuka kwa shangwe, wakimuomba arejee kuipongeza timu hiyo ambayo katika msimu wa 2018/19 ilichukua ubingwa wa ligi Kuu Tanzania Bara.

Huku akizungumzia watu kuwa na furaha amesema, “Mfano sisi mashabiki wa Simba kwa furaha tuliyo nayo kwa kuifunga Nkana na kutinga hatua ya makundi huku tukizingoja kwa hamu kubwa Sh1.3 bilioni.”

Maneno hayo yaliamsha shangwe kanisani hapo lakini askofu huyo alicheka alipotakiwa kurejea kauli hiyo.

Amesema duniani kuna furaha za aina nyingi, ndogo na kubwa huku akitolea mfano ushindi wa Simba kwamba ni mdogo lakini ni muhimu.

Simba imetinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika kwa jumla ya magoli 4-3, baada ya mechi ya kwanza iliyochezewa Zambia kukubali kipigo cha goli 2-1.

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz