Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu atabiri kasi ya maendeleo chini ya Samia

5b36a9a5b85917072b47a2a8edca3a03 Askofu atabiri kasi ya maendeleo chini ya Samia

Sun, 4 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

ASKOFU Mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphori Mkude amesema Tanzania itafanya maajabu mengi makubwa ya maendeleo chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa amani na utulivu .

Alisema hayo kwenye Ibada ya Ijumaa Kuu Maadhimisho ya Njia ya Msalaba ikiwa ni kumbukizi ya mateso ya Bwana Yesu Kristo kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrice mjini Morogoro.

Askofu Mstaafu Mkude alishirikiana pia na Msimamizi wa Jimbo hilo , Monsinyori Lazarus Msimbe pamoja na mapadri wa kanisa hilo.

Alisema Watanzania wanawajibika ipasavyo kuwasaidia viongozi bila kujali dini, rangi , jinsia , itikadi na katika hali hiyo chini ya Rais Samia mambo mengi makubwa ya maendeleo yatapatikana.

" Kwa sasa ni wajibu wetu kumshukuru Mungu na tutende yaliyo mema kwani Katiba yetu imeweka mambo mazuri ya kuweka bayana , hivyo yatupasa tumsaidie Rais afanye kazi zake, " alisema Askofu Mstaafu Mkude.

Alisema bado watanzania wana majonzi kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais John Magufuli ambaye wakati wa uongozi wake aliweze kuharakisha maendeleo ya Taifa katika nyaja mbalimbali za kijamii na kiuchumi

"Tunapomaliza Juma la Kwaresima , tunatambua tuna msiba wa aliyekuwa Rais Dk John Magufuli ,tunatambua aliyotenda na amewavuta watu wengi baada ya kufa kwake , yale aliyoyatenda basi sisi tunamwombea kwa Mungu na pia amsamehe makosa yote kama alikosea na ampokee Mbinguni," alisema Mkude .

Chanzo: www.habarileo.co.tz