Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu asisitiza amani kwa Watanzania

Kofu Pic Joseph Bundara amesisitiza amani nchini

Sun, 17 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askofu wa Kanisa la Pentecostal Holiness Association Mission, Joseph Bundara amesisitiza amani na upendo kwa Watanzania akisema huo ndiyo msingi wa maendeleo na utulivu unaotakiwa.

Askofu Bundara ametoa kauli hiyo leo leo Jumapili Aprili 17, 2022 wakati akihubiri kwenye ibada ya Pasaka katika kanisa hilo Usharika wa Bethania Ipagala jijini Dodoma ambapo amesema amani ikichezewa ni vigumu kuipata.

Askofu Bundara amesema amani ni tunu ambayo Watanzania wamepewa na Mwenyezi Mungu lakini kuna nchi zinaitamani ingawa kwa namna ilivyo haziwezi kuipata kutokana na aina ya maisha wanayoishi hivyo akasisitiza Watanzania kutolewa sifa na kuichezea bahati hiyo.

Bundara ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Tanzania, amesema kuilinda amani kwa gharama hakuhitaji watu kupigana, bali ni utashi na maamuzi huku akisisitiza kutolewa elimu zaidi kwa kizazi kinachokua ili nao watambue nchi imetoka wapi.

Amesisitiza upendo kwa watu wote bila kujali ukabila, udini wala rangi ya mtu kwa kuwa sivyo tulivyolelewa na waasisi wa Taifa na kwamba tunapochezea vitu hivyo ni sawa na kuwadharau na kuyaacha mazuri yote waliyoyaanzisha.

“Lazima tuenzi mazuri yaliyofanywa na waasisi wa nchi hii, hatuwezi kuchezea amani hivihivi wakati tunajua madhara yake, angalieni mataifa mengine ambayo hayana amani inavyowapa shida kuisaka amani na hata upendo kwao haupo tena,”amesema Bundara.

Advertisement Amewataka wanasiasa kuwa makini hata kuchunga ndimi zao ili zisijekuwa chanzo cha kuiondoa amani hiyo ambayo ni faida kwao, siasa zao na hata watoto wao kwani watakuwa wakikua na kuikuta misingi imara imewekwa.

Amewaomba Watanzania kumuombea na kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan ili aendelee kutekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa jambo alilosema linaiweka Tanzania kwenye ramani ya mafanikio zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live