Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu akumbusha kujiandikisha kwenye daftari la Mpiga kura

89926 Kujiandikishapic Askofu akumbusha kujiandikisha kwenye daftari la Mpiga kura

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Tanzania, Jackson Sosthenes amewahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura akisema mwaka 2020 ni muhimu kwa Taifa kwa kuwa linakwenda kwenye uchaguzi mkuu.

Askofu Sosthenes ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba 25, 2019 alipokuwa akitoa ujumbe wa Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Mt Albano lililopo eneop la Posta jijini Dar es Salaam.

Amewaasa waumini wa kanisa hilo na wananchi kuwa mwaka 2020 kutakuwa na uchaguzi wa kuwachagua viongozi kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na urais, ni vyema wakajiandikisha na kupata  fursa kuchagua viongozi makini na wenye sifa kwenye mchakato huo.

“Anglikana Dar es Salaam inahamasisha watu kujiandikisha na tunawatia moyo wagombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo. Ni vyema pia wakawachagua viongozi bora wenye hekima na walio na utayari wa kuwatumikia.

“Kinachomfanya mtu aitwe kiongozi ni namna  anavyowaongoza watu wake. Kiongozi imara siyo yule anayetoa hotuba nzuri na kupendwa bali anayetekeleza matarajio ya wananchi wake,” amesema Askofu Sosthenes.

Katika ibada hiyo, askofu huyo pia alitumia nafasi hiyo kuwasihi wananchi wanaoishi maeneo  kuhama ili kuepukana na changamoto ya mafuriko ambayo yamekuwa yakisababisha madhara mbalimbali katika maeneo hayo.

Chanzo: mwananchi.co.tz