Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu ahimiza kushiriki furaha na wenye uhitaji

1f8291cc80cbff811dab241527861bc5 Askofu ahimiza kushiriki furaha na wenye uhitaji

Sun, 3 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KANISA la TAG la Upendo Revival Christian Center Dodoma limeazimisha siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa kushiriki chakula cha mchana na wajane,yatima na watoto wanaotoka katika mazingira magumu.

Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Dk Salum Vangasiti akizungumza na waumini waliokuwepo katika ibada ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo alisema kushiriki furaha na watu wenye uhitaji ni sehemu ya Ibada.

Mchungaji Dk Salum alisema Kanisa lina wajibu wa kuhakikisha linafanya kazi kubwa katika jamii ambayo ni ya kuokoa roho za watu na kuhakikisha wanabarikiwa kimwili.

"Kanisa letu limeona kuwa ni vyema siku kama ya leo (juzi) ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo ni vyema kufanya ibada ya kushirikiana na makundi mbalimbali ya watu wasiojiweza,yatima na wajane.

" Yesu Kristo anasema kuwa ibada iliyo njema ni pamoja na kuwajali watu wenye uhitaji kama tulivyofanya sisi licha ya kushirikia nao chakula cha pamoja bila kujali itikadi za dini pia tunatoa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha"alisema Mchungaji Dk Salum.

Akizungumzia habari ya amani ya nchi amewataka viongozi wote wa kisiasa,kidini pamoja na taasisi mbalimbali kufanya kazi zao kwa uadilifu sambamba na kutoa haki kwa kila mmoja.

"Ili uweze kuwa kiongozi mzuri ni lazima ufanye kazi kwa misingi ya utii wa Kimungu pamoja na kujiondoa katika masuala ambayo yanaweza kukunyima ujasiri wa kutoa maamuzi.

" Kiongozi ambaye hatendi haki wala atoe maamuzi ya haki kamwe hawezi kujisimamia na hawezi kuwa na ujasiri wa kutoa haki kwa wale ambao wanaonewa"alisisitiza Dk Salum.

Akizungumzia viongozi wa kisiasa amewataka kuhakikisha wanatunza amani ya nchi pamoja na kufanya kazi kwa masilahi mapana kwa taifa na wananchi wake.

Chanzo: habarileo.co.tz