Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu afunguka Magufuli alivyogusa wanyonge

F26d4087a902b8b577d6f760ede993f8 Askofu afunguka Magufuli alivyogusa wanyonge

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

ASKOFU Mstaafu wa Jimbo Katoliki Morogoro, Mhashamu Telesphori Mkude amesema Rais John Magufuli aligusa maisha ya Watanzania hasa wanyonge na aliharakisha maendeleo ya Taifa kijamii na kiuchumi.

Askofu mstaafu Mkude, alisema hayo jana mjini Morogoro wakatoa akitoa pole kwa Watanzania kutokana na kifo cha Rais wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Magufuli.

Alisema, Rais Magufuli atakumbukwa kwa kutoa kipaumbele katika elimu, na hadi sasa mfumo wa elimu bila malipo kwa wanafunzi umesaidia wazazi wafanye shughuli zao za kujiongezea kipato badala ya kuwaza gharama za kusomesha watoto.

Askofu mstaafu Mkude alisema, Rais Magufuli alithubutu kutoa uamuzi wa papo kwa papo ili kusaidia maendeleo kwa haraka kwa maslahi ya taifa zima, na hakuwa na ubaguzi katika kuongoza wananchi katika usawa usiojali maslahi ya chama na ukabila.

Alisema Rais Magufuli, alikuwa mcha Mungu aliyethubutu kutetea wanyonge na alimuamini Mungu kwa kila jambo.

Aliwaomba viongozi waliopo madarakani kushikamana kuendeleza mafanikio yalioachwa na Magufuli ili kuwapa Watanzania tumaini jipya, na kwamba huu si wakati wa kunyoosheana vidole.

"Tunapaswa kumuombea Rais wetu wa sasa mama Samia Suluhu Hassan aweze kuongoza Watanzania kwa kuiga mfano wa Dk Magufuli ambaye sasa amepumzika katika usingizi wake wa milele" alisema Askofu Mstaafu Mkude.

Msimamizi wa Jimbo Katoliki Morogoro, Monsinyori Lazarus Msimbe, aliwaomba Watanzania wamuombee Magufuli kwa Mungu ili amsamehe na kumpokea katika ufalme wake.

Msimbe alisema pia Watanzania wanapaswa kuombea umoja na mshikamano kwa maendeleo ya Taifa na akashauri viongozi waenzi juhudi za Magufuli zikiwemo na kupambana na rushwa na ufisadi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz