Dini

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Shoo wa KKKT aja na waraka

53259 Pic+shoo

Sat, 20 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo ametaja athari zitakazojitokeza kama Wakristo na Watanzania hawatatembea na Mungu.

Katika waraka wa pasaka wa 2019, Askofu Shoo ametaja athari hizo kuwa ni vita, ubabe, chuki, visasi, kutovumiliana, kutoheshimiana na hatimaye kusambaratika kwa uhusiano mwema na Mungu.

Askofu Shoo ametoa waraka huo wenye kurasa nne kama mkuu wa kanisa, tofauti na waraka wa pasaka wa mwaka jana uliosainiwa na maaskofu 27 wa KKKT uliobeba ujumbe mzito kwa Taifa.

Waraka huo ilibeba ujumbe huo ulitahadharisha juu ya kushamiri kwa chuki mioyoni mwa watu ambalo ni chimbuko la visasi, kukata tamaa na ushiriki mdogo wa wananchi katika chaguzi.

Pia ulizungumzia matukio ya utekaji, utesaji, kupotea kwa watu na kushamiri kwa mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa na mauaji yenye mwelekeo huo.

Lakini katika waraka wa 2019, umejikita zaidi katika mafundisho ya Mungu na uhusiano wake na wanadamu.

“Ujumbe ni Mungu ametupatanisha naye kwa njia ya Yesu. Tuishi kwa kupatana licha ya tofauti zetu. Yako ya msingi tunayopaswa kuyazingatia na kuyaheshimu ili tuweze kutembea na Mungu,” alisema Askofu Shoo.

“Kutembea pamoja kama wanandoa, familia, jamii na Taifa. Tusipozingatia misingi ya kutembea pamoja matokeo yake ni vita, ubabe, chuki, visasi, kutokuvumiliana na kutokuheshimiana.”

Alisema, “penye upatanisho pana haki, amani, uwazi na ukweli. Ujumbe wa pasaka unatuhumiza kuthamini huduma ya upatanisho alioufanya Mungu mwenyewe kupatana nasi kwa njia ya Yesu Kristo.

“Yesu mwenyewe kwa unyenyekevu wote alikubali kuwa mpatanishi ili atupatanishe sisi na Mungu na kwa ajili yake tujifunze kupatana, kupendana na kuvumiliana sisi kwa sisi.”

Katika hatua nyingine, Askofu Shoo katika waraka huo amezungumzia suala la uharibifu wa mazingira linalochangia mabadiliko ya tabia nchi ikiwamo kukosekana kwa mvua na kuongezeka kwa joto.



Chanzo: mwananchi.co.tz